KCB BANK TANZANIA YAZINDUA ZED 360 KUBORESHA UKUSANYAJI WA ADA SHULENI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, September 17, 2026

KCB BANK TANZANIA YAZINDUA ZED 360 KUBORESHA UKUSANYAJI WA ADA SHULENI

BAGAMOYO, Tanzania – 17 Septemba 2026 – KCB Bank Tanzania imezindua rasmi mfumo wa kidijitali wa ZED 360, unaolenga kuboresha ukusanyaji wa ada, upatanisho wa malipo na usimamizi wa taarifa za kifedha katika taasisi za elimu nchini.

Mfumo huo umebuniwa kusaidia shule kukabiliana na changamoto mbalimbali katika usimamizi wa mapato, ikiwemo ugumu wa kufanya upatanisho wa malipo (payment reconciliation), ufuatiliaji wa makusanyo, utunzaji wa kumbukumbu za kifedha na upatikanaji wa taarifa kwa wakati halisi.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ZED 360, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Cosmas Kimario, alisema benki hiyo inaendelea kumweka mteja mbele kwa kutumia teknolojia kuleta suluhisho zinazorahisisha shughuli za kila siku kwa makundi mbalimbali ya wateja.
Kupitia ZED 360, shule zitapata uwazi mkubwa zaidi katika usimamizi wa mapato yao, kupunguza utegemezi wa michakato ya mikono na kufanya maamuzi kwa kutumia taarifa sahihi zinazopatikana kwa wakati halisi. Mfumo huu umeundwa kuboresha ufanisi na kuongeza uwajibikaji katika taasisi za elimu,” alisema Kimario.
ZED 360 Yarahisisha Usimamizi wa Ada

ZED 360 inarahisisha mchakato mzima wa usimamizi wa ada, kuanzia utoaji wa ankara, ukusanyaji wa ada, upatanisho wa malipo hadi utoaji wa taarifa za kifedha kwa wakati halisi.

Mfumo huo pia unalenga kurahisisha maisha ya wazazi na walezi kwa kuwawezesha kupokea ankara za ada kwa urahisi na kufanya malipo kupitia njia mbalimbali za kidijitali na kifedha.
Kupitia ZED 360, wazazi na walezi wanaweza kulipa ada kupitia matawi yote ya KCB Bank Tanzania, KCB Mobile App, mawakala wa KCB pamoja na mawakala wa Mixx by Yas kote nchini.

Teknolojia Katika Mageuzi ya Sekta ya Elimu

Uzinduzi wa ZED 360 ni sehemu ya mkakati wa KCB Bank Tanzania wa kuendelea kuwekeza katika mageuzi ya kidijitali, kwa lengo la kuboresha uzoefu wa wateja, kuongeza ufanisi wa shughuli za taasisi na kuchangia maendeleo ya sekta mbalimbali za uchumi.

Katika sekta ya elimu, suluhisho hilo linatarajiwa kusaidia taasisi kuwa na mifumo yenye uwazi zaidi katika usimamizi wa mapato na taarifa za kifedha, huku ikiwezesha uongozi wa shule kupata taarifa muhimu kwa wakati na kufanya maamuzi yanayozingatia takwimu.

KCB Bank Tanzania pia imewashukuru uongozi wa Shule ya Marian kwa kushiriki katika majaribio ya awali ya mfumo huo, ambayo yalisaidia kutoa mrejesho muhimu katika kuboresha ZED 360 kabla ya uzinduzi wake rasmi.

KCB Yatoa Wito kwa Taasisi za Elimu

KCB Bank Tanzania imezihimiza taasisi za elimu nchini kutumia fursa ya teknolojia ya ZED 360 kuboresha usimamizi wa ada, kuongeza uwazi katika mifumo ya kifedha na kuimarisha utoaji wa huduma za elimu.

Kwa kuunganisha ukusanyaji wa ada, upatanisho wa malipo na taarifa za kifedha katika mfumo mmoja wa kidijitali, ZED 360 inalenga kusaidia shule kuwa na usimamizi wenye ufanisi zaidi wa mapato na taarifa zao za kifedha.
















at 20:10

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages