Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine
Mahiga akisalimiana na Bw. Luca Neghesti kutoka SportPesa Tanzania leo ofisini
kwake jijini Dar es Salaam. Bw. Neghesti amefuatana na wawakilishi wa timu ya
Mpira wa Miguu ya Everton ya nchini Uingereza kumpa taarifa Mhe. Waziri kuhusu
maandalizi ya kuileta timu hiyo kucheza mechi za kirafiki nchini Tanzania hivi
karibuni.
Mhe.
Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa timu ya mpira ya
Everton ya nchini Uingereza. Timu hiyo ipo katika hatua za mwisho za maandalizi
ya kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki. Mhe. Waziri alisema
ziara hiyo itasaidia kuitangaza Tanzania duniani pamoja na kuhamasisha mchezo
wa mpira wa miguu kwa vijana wa Kitanzania. Anaozungumza nao kutoka kulia ni
Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu
hiyo, Bw. David Harrison; Mkuu wa Ulinzi na Usalama (Head of Safety and
Security) wa timu, Bw. Dave Lewis na Bw. Alan Chisholm kutoka Thomas
Cook.
Waziri
Mahiga akifurahia zawadi ya jezi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Uendeshaji wa Mpira
wa Miguu (Head of Football Operations) wa timu ya Everton, Bw. David Harrison.
Jezi hiyo ni ya Mchezaji wa Timu hiyo ambaye pia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya
Ireland, Bw. Coleman.
Picha
ya pamoja.
No comments:
Post a Comment