CRDB yachomoza kwa usalama duniani - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, October 12, 2017

CRDB yachomoza kwa usalama duniani


Benki ya CRDB imetajwa miongoni mwa taasisi salama zaidi za fedha duniani, hivyo kuiweka Tanzania miongoni mwa nchi 11 kutoka Afrika zilizokidhi vigezo hivyo.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya Globa Finance ulihusisha nchi 106 na taasisi husika zikawekwa kwenye makundi ya benki 50 salama zaidi duniani, benki 50 za biashara salama zaidi duniani, benki 50 salama zaidi kutoka nchi zinazoibukia kiuchumi, benki salama zaidi ya Kiislamu na benki bora kwa kanda ya Afrika, Asia, Ulaya, Mashariki ya Mbali na Amerika.

Kukidhi vigezo na kuwemo kwenye orodha hiyo, Benki 1,000 kubwa zaidi zilifanyiwa tathmini kwa kuzingatia vigezo tofauti.

Mkurugenzi wa idara ya habari wa Global Finance, Joseph Giarraputo amesema kulikuwa na changamoto wakati wa kukamilisha mchakato huo na hasa kwa benki zenye matawi kwenye zaidi ya nchi moja na zinahudumia wateja wenye ofisi katika mataifa tofauti.

“Licha ya juhudi tulizozifanya kuzihuisha, kanuni za uendeshaji wa benki zimekuwa tofauti kwa kila nchi kutokana na changamoto zilizopo pamoja na rasilimali,” amesema Giarraputo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa amesema ushirikiano wa wafanyakazi wa taasisi hiyo ndiyo chachu ya mafanikio ndani na nje ya mipaka.

“Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa huduma bora kwa mteja. Usalama wa taarifa za wateja wetu ni kitu kinachopewa kipaumbele.

Hii ni kwa maeneo yote; mikopo, huduma za mtandaoni hata kwa simu za mkononi,” amesema Mwambapa.

Licha ya CRDB yenye thamani ya Sh5.49 trilioni, taasisi tatu kutoka kaskazini mwa Afrika nazo zimetajwa.

Hizi ni National Bank of Egypt (Misri), Attijariwafa Bank ya Morocco na Arab Tunisian Bank ya Tunisia.

Kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, kuna Banco Angolano de Investimentos ya Angola, Rawbank ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Standard Bank ya Afrika Kusini, GCB ya Ghana, Zenith ya Nigeria, Ecobank ya Togo na Stanbic ya Kenya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages