Makonda akiuliza jambo la kiutaalamu kuhusu meli hiyo kwa baadhi ya makampeni wa meli hiyo mara baada yakuwasijilijijini hapa kwakutoa matibabu bure
Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri ya China yenye Hospital
ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha
kwaajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es
Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea
Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa ambapo ndani yake
vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya
Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.
Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwaajili ya wagonjwa
ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii
iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.
RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa
Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa
umeshindikana.
Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana,
Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili ya kukarabati na kufunga vifaa
vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.
Amesema *lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi
anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.
Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda
mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka
China.
Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN
BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo
wananchi Wajitokeze kwa wingi.
















No comments:
Post a Comment