Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa
kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na
mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.
Wawili hao walifunganishwa katika ndoa mbele ya Malkia na wageni 600
waliokuwemo ndani ya kanisa la St George, katika Windsor Castle.
Bi Markle alikuwa amevalia vazi la harusi lililoshonwa na fundi mbunifu wa mitindo Mwingereza Clare Waight Keller.
Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani
ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari
hilo na kuingia kanisa la St George.
Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.
George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle baadaye walipitia kwenye mji wa
Windsor kwa msafara kwa kutumia kigari maalum cha kuvutwa na farasi.
Harry, ndiye aliyeyemsindikiza Bi Markel kwenda kwenye madhabahu baada
ya babake Thomas kushindwa kuhudhuria harusi hiyo kutokana na sababu za
kiafya.
Mkesha wa harusi, Mwanamfalme Harry, 33, aliambia umati wa watu Windsor
kwamba anajihisi "mtulivu" na kwamba Bi Markle, 36, anajihisi "vyema
sana".
Katika kiapo chake cha ndoa, Bi Markle hakuahidi "kumtii" mume wake. Mwanamfalme Harry ameamua kuwa na pete ya ndoa.
Wageni 600 walifuatilia harusi hiyo, ambayo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, katika kanisa la St George.
Umati wa watu wakiungana na waandishi wa habari kutoka maeneo mengi duniani wamlikusanyika Windsor kwa sherehe hii kubwa.
Inakadiriwa kwamba watu hadi 100,000 walikuwa kwenye barabara za mji huo.
Watu wa kawaida 1,200, wengi ambao wametambuliwa kwa juhudi zao za
hisani katika jamii, walialikwa kuhudhuria harusi hiyo Windsor Castle.
Bi Markle alikuwa na mabinti 10 wapamba harusi na wavulana, wote wa
chini ya miaka minane, wakiwemo Mwanamfalme George na Bintimfalme
Charlotte.
Bi harusi alilakiwa na Mwanamfalme Charles, ambaye alimtembeza hadi kwenye madhabahu.
Wakati wa ibada, wawili hao walikula kiapo kila mmoja akijitoa kwa
mwenzake na kusema: "kwa mema, kwa mabaya, kwa ujatajiri, kwa umaskini,
kwa ugonjwa na kwa afya, kukupenda na kukuenzi, tangu kifo
kitutenganishe."

No comments:
Post a Comment