RC Makonda Kupokea Makontena 10 Kutoka Marekani - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 20, 2018

RC Makonda Kupokea Makontena 10 Kutoka Marekani

Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel Subash Patel akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. 
 Sehemu ya kiwanda cha MMI Steel .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari.
Rc Makonda akipokea Mabati 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi venye thamani ya milioni 400 kutoka kiwanda cha MMI Steel kwa ajili ya kufaniksha ujenzi wa nyumba za walimu.

Akizungumza katika hafla ya kupokea vifaa hivyo jijini Dar es Salaam Mhe. Makonda amesema kuwa kiwanda hicho kimetoa msaada wa mabati 15,000 yenye thamani ya milioni 360 pamoja nondo tani 22.

Mhe. Makonda amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukamilisha nyumba za walima ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki.

“Watanzania wanapaswa kuiga mfano huu katika kuchangia sekta ya elimu ili mkoa wetu endelee kufanya vizuri”amesema Mhe. Makonda.

Mhe. Makonda amesema tayari wameanza kuchukua vifaa hivyo vya ujenzi kutoka kiwandani kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa nyumba za walimu.

Ameeleza kuwa kila mtu anatakiwa kuunga mkono juhudi za kiwanda jambo ambalo litafanikisha maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Katika hatua nyengine Mhe. Makonda amebainisha kuwa kuna makontena 10 ya vitabu ambavyo vinatarajia kuja nchini kutoka marekani kwa ajili ya mktaba ya kisasa ambayo itafanikisha maendeleo ya elimu.

“Kuna makontena 10 ya vitabu pamoja na vifaa vya maabara ambavyo ni msaada kutoka marekani vinatarajia kuja nchini ”amesema Mhe. Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha MMI Steel Subash Patel, amesema kuwa ametoa msaada wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuchangia sekta ya elimu katika mkoa wa Dar es Salaam.

Patel amesema kuwa katika kiwanda chake kuna wafanyakazi 3,000 ambao wana ajira ya moja kwa moja, huku asilimia kubwa kati yao wanawatoto wanaosoma.

Ameeleza kuwa kutokana hilo ameona ni vyema kuwachangia katika kufanikisha ujenzi wa nyumba za walimu.

“Nitaendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha masula mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo kazi ya kujenga nyumba za walimu”amesema Patel.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa atatoa msaada mwengine wa rangi katika kufanikisha ujenzi wa nyumba za walimu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages