Tanzia : MWANDISHI WA HABARI STEPHEN KIDOYAYI AFARIKI DUNIA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 17, 2018

Tanzia : MWANDISHI WA HABARI STEPHEN KIDOYAYI AFARIKI DUNIA


Stephen Kidoyayi enzi za uhai wake

Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) unasikitika kutangaza kifo cha mwandishi wa habari Stephen Kidoyayi kilichotokea jana Jumatano Mei 16, 2018.
Stephen Kidoyayi ambaye alikuwa anaandikia gazeti la Jamboleo kabla ya kuhamia gazeti la Tanzanite na pia alikuwa mwalimu wa Buhangija Sekondari amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga alipofikishwa leo baada ya kuugua.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu,amesema baba yake takribani siku nne alikuwa anaumwa na leo asubuhi alifikishwa hospitali akisumbuliwa na kifua/kukohoa na ilipofika saa saba mchana akafariki dunia.
Msiba upo nyumbani kwake Buhangija mjini Shinyanga na taratibu za mazishi zinaendelea,taarifa zaidi zitatolewa.
Stephen Kidoyayi ni miongoni mwa waandishi wa waandishi wa habari waanzilishi wa Shinyanga Press Club,na amewahi kuwa katibu mtendaji wa Shinyanga Press club na mpaka umauti unamfika alikuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shinyanga Press club.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Stephen Kidoyayi.Amina!

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages