Yusuph Mlela Amtolea Povu Zito Steve Nyerere Kisa Mzee Majuto - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, May 3, 2018

Yusuph Mlela Amtolea Povu Zito Steve Nyerere Kisa Mzee Majuto


Muigizaji wa Bongo movie Yusuph Mlela amemjibu muigizaji mwenzake na mwanasiasa Steve Nyerere baada ya kumtuhumu yeye na wasanii wenzake kwa kutafuta kiki Kupitia Mzee Majuto.

Steve Nyerere aliwajia juu wasanii wote walipoenda hospitali kumuona Mzee Majuto na kupiga naye picha kisha kuweka Kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kutafuta kiki.

Lakini pia Steve aliwatuhumu wasanii hao kwa kuenda kumtembelea hospitalini hapo lakini hawa cha hii chochote Kwenye kitabu chake cha matibabu mwisho wa siku wanaishia kupata tu kiki.

Baada ya Tuhuma hizo, Yusuph Mlela akiwa ni miongoni mwa wasanii walioenda kumuona Mzee Majuto na kisha kupiga naye picha amemtolea povu zito Steve Kupitia kipindi cha Enews ya EATV:

"Steve Nyerere ni Steve Nyerere sasa sijui alitaka akamuone mwenyewe ili hili tatizo lionekane lake peke yake, sijui wakati hilo suala ni la kwetu sote lakini sijajua yeye mwenyewe alimaanisha nini, maana siwezi kukaa nikaanza kulumbana naye maana nina vitu vingi sana vya kufanya lakini mimi nilifanya kwa ajili ya upendo na mzee”.

Mzee Majuto yupo safarinishwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages