MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT JIJINI DAR ES SALAAM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 8, 2018

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu baadhi ya watoto walioletwa kwa matibabu katika hospitali ya CCBRT kama wagonjwa wa nje,kulia anayetoa maelezo ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa CCBRT Bw. Erwin Telemans. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Luke Maulid mwenye umri wa miaka 4 kutoka Mtwara ambaye anapata matibabu ya mguu katika hospitali ya CCBRT.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Binti wa miaka 11 anayefahamika kwa jina la Maureen Mbilinyi mkazi wa Mbezi ambaye anapata matibabu ya kuondoa uvimbe jichoni katika hospitali ya CCBRT.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bibi Helena Mjinja mwenye umri wa miaka 64 kutoka Musoma anayepata matibabu ya Fistula katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanawake ambao wamepata matibabu ya Fistula na kupona na kisha kufundishwa kazi za mikono katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw.Erwin Telemans juu ya utengenezaji wa viungo bandia vinavyotengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia watoto Mussa Hussein (kulia) mwenye umri wa miaka 8 mkazi wa Kigamboni na Abdul Hamad (kushoto) mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Yombo Vituka wakicheza mpira kwa kutumia miguu maalum, Makamu wa Rais jana alifanya ziara kwenye hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa macho bandia kutoka kwa Mtaalamu wa Macho wa Hospitali ya CCBRT Bi. Rehema S. Semindu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi na wagonjwa wa hospitali ya CCBRT mara baada ya kumaliza kutembelea hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages