Waziri wa Mazingira January Makamba akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya MABAKI MALI Irene Muja alipotembelea Banda hilo kujionea shughuli za Uzalishaji Mali na Utunzaji wa Mazingira Zinazofanywa na Kampuni hiyo.
Waziri wa Mazingira January Makamba akiongea na Wajasiliamali wa Bidhaa za Majumbani kwa kutumia Mabaki ya Bidhaa mbalimbli katika banda la kampuni ya Aisha Kipepeo katika Maonyesho ya wiki ya Mazingira Mnazi Mmoja jijini Dsm (kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Magdalena Mshamu, anayefata ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kuzalisha Nishati ya Mkaa utokanao na Maganda ya Ndizi ya Green Conservers Baraka Machumu, na Mkurugenzi wa Kampuni ya Aisha Kipepeo Bi Aisha Kibiriti.)
Wakati Maonyesho ya wiki ya Mazingira yanafikia ukingoni Waziri mwenye dhamana na mazingira January Makamba ametoa pongezi kwa Wajasiliamali wadogo wanaojihusisha na Utunzaji wa Mazingira.
Akiongea alipotembelea maonyesho hayo siku moja kabla ya kufungwa kwa maonyesho hayo Majaliwa amewapongeza wajasiliamali wadogo kutoka katika Kampuni ya MABAKI MALI na AISHA KIPEPEO wanaotengeneza bidhaa za Majumbani kwa kutumia Mabaki ya bidhaa mbalimbali na taka.
Amesema Amefurahishwa Kuona Vijana hasa wa Kike wanapata Muamko wa kuona Fulsa inayopatikana katika kuhifadhi na kutunza mazingira hasa kwa Kuzalisha Bidhaa Mbalimbali kutokana na Taka na Mabaki ya Bidhaa Mbalimbli.
Akiongea Wakati wa Kufunga Maonyesho hayo Mkurugenzi wa Kampuni ya MABAKI MALI Irene Muja, amesema aefurahishwa sana kwa Kutembelewa na Waziri huyo na kwamba imewapa motisha wa kufanya vizuri Zaidi.


No comments:
Post a Comment