BENKI Ya KCB imewezesha kwakutoa Shilingi milioni 30 katika sherehe ya shukrani ya Marian Schools, iliyojumuisha mbio za miguu, matembezi, na misa ya shukrani.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki hiyo Cosmas Kimario na Mgeni rasmi wa sherehe hizo, aliipongeza Taasisi za Marian kwa mafanikio makubwa waliyoyafikia kielimu, kijamii, na kiuchumi.
Kimario alisisitiza kuwa tangu kuanzishwa mwaka 1997, Taasisi za Marian zimeonyesha dhamira thabiti ya kutoa elimu bora na kuzalisha wahitimu wenye mchango mkubwa katika jamii na tija kazini.
Aliendelea kwa kueleza jinsi Marian ilivyopanua shughuli zake kutoka shule moja, Marian Girls Secondary School, hadi kuwa na shule tatu za sekondari, zahanati, hoteli, na chuo kikuu (Marian University), kilichoanzishwa mwaka 2014.
Mafanikio haya yameleta mabadiliko chanya katika elimu, jamii, na uchumi wa taifa. Wahitimu wa Marian Schools wameiva kielimu na kinidhamu, wakitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Meneja wa Shule za Marian Valentine Bayo alitoa historia fupi ya Taasisi za Marian, akisema: "Mnamo mwaka 1991 nilitumwa hapa na wakubwa wangu wa Shirika la Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) kama padre kijana kwa kazi ya uinjilishaji.
Kutokana na hali ya uduni wa eneo hili ambalo lilikuwa limesahaulika, tulianzisha juhudi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha shule za chekechea na ufundi. Hatimaye, juhudi hizi zilipelekea kujengwa shule ya sekondari ya wasichana ya Marian mnamo mwaka 1997.
Aidha katika ushirikiano kati ya Benki ya KCB na Taasisi za Marian kati ya mwaka 2021 na 2024, KCB Bank imewekeza katika miradi mbalimbali ya Taasisi za Marian, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa shule za Marian Girls na Marian Primary, ujenzi wa majengo ya ghorofa sita kwa ajili ya madarasa na hosteli za Marian Boys School, na kuchangia baadhi ya gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.
Sherehe hizi pia zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Askofu Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Zanzibar, Agustine Shao; Mkuu wa Shirika la Holy Ghost, Mhe. Shauri Selenda; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo; Meneja na Mwanzilishi wa huuShirika la Roho Mtakatifu; wenyeviti wa bodi za Taasisi za Marian; pamoja na wazazi, wanafunzi, na wafanyakazi wa taasisi hizo.
No comments:
Post a Comment