Hayo yamesemwa leo Nov, 07, 2024 Jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ambapo Mkenda amesema kuwa miundombinu hii ni ya kisasa na inaendana na Azma ya Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dkt Samia Saluhu Hasana ya kutaka huduma muhimu ya uthibiti wa matumizi ya Nyuklia ipelekwe karibu na Wananchi.
Uzinduzi wa Maabara hiyo utaenda sambamba na uzinduzi ya Jengo la Ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) na utafanyika tarehe 11 Novemba, 2024 Dunga Zuze visiwani Zanzibar.
Waziri Mkenda ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa wataalamu wa Sayansi ya nguvu za Nyuklia, kupitia ufadhili wa Samia Scholarship Extended Watanzania watano wamepata Ufadhili huo na wanaenda kusomea taaluma hiyo katika Nchi za Austria, Afrika Kusini, Uingereza, Canada na Italia katika Vyuo Vikuu Bora vinavyotoa mafunzo ya Teknolojia ya Nuklia.
Akizungumza katika Mkutano huo Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia QS Omar Kipanga amesema Teknolojia ya Nyuklia ina manufaa mengi katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya , Kilimo nakusisitiza kuwa Wizara inaendelea kuimarisha Uthibiti wa matumizi yake na kuhimiza matumizi sahihi katika maendeleo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC Prof Joseph Msambichaka amesema Taasisi hiyo inaendelea na juhudi za kutoa Elimu kwa Umma juu ya Taasisi hiyo na faida za teknolojia.
No comments:
Post a Comment