VIONGOZI Wateule walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakipitia hati zao za kiapo kabla ya kuapishwa leo 14-11-2024 (kushoto) Mhe. Iddi Said Khamis, ameteuliwa kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar na Ndg. Hiji Dadi Shajak, ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.
BAADHI ya Waalikwa na Wanafamilia wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Viongozi waliotwa hivi karibuni, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwaapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Iddi Said Khamis kuwa Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Hiji Dadi Shajak,kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 14-11-2024 na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewaapisha viongozi wawili aliowateua hivi karibuni.
Viongozi walioapishwa ni Mhe. Iddi Said Khamis, Kadhi wa Mahkama ya Kadhi ya Rufaa baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dk. Mwinyi tarehe 24, Oktoba 2024.
Kabla ya uteuzi huo, Kadhi Iddi Khamis alikuwa Mrajis wa Mahkama ya Kadhi Zanzibar.
Mwengine ni Ndg. Hiji Dadi Shajak, Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kabla ya wadhifa huo, Ndg. Shajak alikua Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kurusha Maudhui, Zanzibar (ZMUX). Aidha, Shajak aliteuliwa Septemba, 25 mwaka 2024 kushika majukumu mapya.
Wakizungumza kwenye hafla ya uapisho huo, iliyofanyika Ikulu, Zanznibar, viongozi hao walimuahidi Rais Dk. Mwinyi kuyafanyia kazi maelekezo yake yote na kuendeleza jitihada ya taasisi mpya wanazozitumikia kwa kuendeleza ushirikiano kwa Serikali na wadau wengine.
Hafla ya uapisho huo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, viongozi wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na Masheikh kutoka Ofisi ya Mufti, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment