DK.Mwinyi: Tuzitumie Rasilimali za Chama Kujijenga Kiuchumi - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Tuesday, December 31, 2024

demo-image

DK.Mwinyi: Tuzitumie Rasilimali za Chama Kujijenga Kiuchumi

20751539-d5d3-4c75-838c-90f111f76b56
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Viongozi wa CCM, akikata utepe kulifungua Jengo la Afisi ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini Kichama, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amezisisitiza Jumuiya za Chama hicho kuzitumia rasilimali vizuri kwa lengo la kukijengea uwezo kiuchumi.

Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozindua Jengo jipya la Afisi ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mfenesini, Wilaya ya Magharibi A.

Aidha Makamu Dk. Mwinyi amefahamisha kuwa Kazi za Siasa zinahitaji fedha nyingi hivyo Chama ni lazima kiwe na Miradi inayozalisha ili kujijenga Kiuchumi.

Makamu Dk.Mwinyi ameupongeza Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kichama Mfenesini kwa Kujenga Jengo la kisasa la Jumuiya hiyo na kuwa na dhamira ya kuanzisha Miradi ya Ushoni na Ukumbi wa shughuli mbalimbali.

Halikadhalika Dk.Mwinyi ameahidi kwa Chama cha Mapinduzi kuunga Mkono Miradi ya Kimkakati ya Itakayoanzishwa na Jumuiya zote za Chama hicho ili ziweze kujitegemea.

Akizungumzia suala la Udhalilishaji wa Kijinsia Dk, Mwinyi ametoa wito kwa jamii Kuanzia ngazi ya Familia kwa kila Mmoja kutimiza wajibu wa kukemea na kukomesha Vitendo hivyo ndani ya jamii.
3f3b731e-d402-4ddb-83ca-d44d20caab75
8e4a7e33-5802-43ca-920d-aff4192894c7
13b1147d-267f-4eae-9666-46d6e3028c99
91edfa31-14ae-43c7-bf34-d414b1e99eaa

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *