
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kinachofanyika jijini Tanga.
- Aipongeza kusimamia kwa ufanisi upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini
- Asema imerahisisha mazingira ya uwekezaji kwenye vituo vya mafuta vijijini na vituo vya CNG
- Aitaka kutathmini kiasi cha upotevu wa maji yanayozalishwa na Mamlaka za Maji nchini
Na.Mwandishi Wetu-TANGA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa usimamizi thabiti wa huduma za nishati na maji nchini ambao ameeleza kuwa umechangia kuleta na kuimarisha utulivu kwenye sekta ya nishati na taifa kwa ujumla.
Biteko ametoa pongezi hizo leo Februari 17, 2025 wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa EWURA kinachofanyika jijini Tanga.
"EWURA mnafanya kazi kubwa ya kudhibiti upatikanaji wa huduma za uhakika za umeme na mafuta nchini kwa ufanisi mkubwa, mmeleta utulivu kwenye sekta ya nishati nchini, mmerahisiha mazingira ya uwekezaji kwenye CNG, vituo vya mafuta vijijini na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwenye nishati safi ya kupikia, nawapongeza sana." Alisema Mhe. Biteko.
Dkt Biteko amesisitiza EWURA kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya kiudhibiti kuhusu ajenda ya misheni 300 ya umeme na kuwasimamia watoa huduma wanaodhibitiwa kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya huduma kwa mteja inayotekelezeka.
Aidha, ameitaka EWURA kuhakikisha inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara ya mafuta nchini, na kushirikisha wadau na watoa huduma wanaodhibitiwa kwenye maamuzi ya kiudhibiti ili utekelezaji wake uwe na tija.
Katika hatua nyingine, ametoa rai kwa EWURA kufanya tafiti za kina kuhusu huduma zinazodhibitiwa ili kubaini maeneo yanayohitaji kutiliwa mkazo, kufanya kazi kwa weledi na kufuata sheria ikiwamo kupokea hoja za wanaokosoa utendaji wa taasisi ili kuisaidia kujitathmini na kuboresha zaidi utendaji wake.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, akizungumza wakati akifungua kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kinachofanyika jijini Tanga.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, akizungumza wakati wa kikao cha nne cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kinachofanyika jijini Tanga.






Picha mbalimbali wakati wa ufunguzi wa kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, kilichofanyika jijini Tanga leo 17/02/24. Kikao hicho kimefunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Mashaka Biteko (Mb).
No comments:
Post a Comment