JUBILEE HEALTH INSURANCE YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE,YAPEWA TUZO YA TSEA 2025 - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Tuesday, April 8, 2025

demo-image

JUBILEE HEALTH INSURANCE YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE,YAPEWA TUZO YA TSEA 2025

WhatsApp%20Image%202025-04-07%20at%2022.01.42
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Jubilee Health Insurance imesema inayofuraha kutangaza mafanikio yake makubwa nchini Tanzania baada ya kupata tuzo ya Service Excellence Awards (TSEA) 2025.

Taarifa ya Jubilee Health Insurance kwa vyombo vya habari imesema tuzo hiyo ambayo imetolewa Machi 28 mwaka huu inawafanya waongeze juhudi katika kutoa huduma bora kwa wateja, jambo ambalo limekuwa kipaumbele chao kila wakati.

Pia wanajivunia sana kupata tuzo hiyo ya heshima, ambayo inadhihirisha kazi ngumu ya timu yao na imani kubwa ambayo wateja wao wanayo kwao.

Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu,” amesema Veronica Nyage ambaye ni Mkuu wa Idara ya huduma kwa Wateja kutoka Jubilee Health Insurance.

Tuzo hii inaonyesha jitihada na kujitolea kwa timu yetu yote, na tumejizatiti kuendelea kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu.

Jubilee Health Insurance itaendelea kuzingatia kuridhika kwa wateja na ubora wa huduma, ikijivunia mafanikio haya na kuhakikisha huduma za afya bora zaidi kwa Watanzania.

"Asante kwa wateja wetu, washirika, na wafanyakazi wetu kwa msaada wao usio na kikomo. Tunatarajia kufikia mafanikio makubwa zaidi pamoja."

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *