RC ARUSHA APOKEA UJUMBE WA MABUNGE DUNIANI (IPU) - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, December 4, 2025

RC ARUSHA APOKEA UJUMBE WA MABUNGE DUNIANI (IPU)

* Kufanya Mkutano wa Mabunge Mkoani Arusha

* Wajumbe zaidi ya 1500 kutoka nchi wanachama wa IPU kuhudhuria

* Rais Dkt. Samia apendekezwa kuwa Mgeni rasmi

Na Mwandishi wetu, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,CPA. Amos Makalla ma ameupokea na kuzungumza na Ujumbe wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha na kuhusisha Maspika, Wabunge na Viongozi zaidi ya 1500 kutoka duniani kote.

Ujumbe wa IPU umeongozwa na Balozi Ande Filip, akiongozana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Geneva,Uswisi Dkt. Hoyce Temu ambapo katika maelezo yake Balozi Ande amesema katika Mkutano huo, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

Tanzania ni Mwenyeji na sababu kubwa ni ushiriki na historia yake katika IPU na kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania na sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa Kihistoria.” Amesema Makalla.
Makalla amesema Mkutano huo ni fursa kwa Wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na ukija wakati mzuri katika kudhihirisha amani, usalama na utulivu uliopo nchini na kuaminika kwa Tanzania Kimataifa, akiwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.
Kwa Upande wake Balozi Ande kwaniaba ya Maafisa wengine wa IPU, amesema Mkutano huo wa Kimataifa utafanyika kwa siku sita Jijini Arusha na kulingana na ratiba, washiriki wake kutoka kote duniani watakuwa na zaidi ya siku sita Mkoani Arusha ili kuwapa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na Vivutio vya Utalii vilivyopo Arusha na maeneo mengine ya jirani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages