Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imesema
itasitisha uzalishaji wa noti ya Tsh 500 kutokana na kuwapo sababu mbalimbali.
Na imefikia uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo na kasoro kwenye noti hiyo.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa
Huduma za Kibenki wa BOT, Abdul Dolla wakati wa semina ya waandishi wa habari
mjini Zanzibar.
Dolla alisema, noti hiyo imeonekana
kuchakaa haraka zaidi, ikilinganishwa na noti nyingine.
Katika hatua nyingine, benki hiyo
imesema itaanza msako wa kuwabaini watu wanaofanya biashara ya maduka ya
kubadilishia fedha ‘Bureau De Change’, ambayo yamekuwa yakifanya kazi ya
kusafirisha fedha kwenda nje ya nchi.
Alisema kuanzia Julai mosi mwka huu,
maduka hayo ambayo hayajafikisha mtaji wa sh milioni 100 yatafutiwa leseni.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya matangazo
na makubaliano yaliyotolewa na kukubaliana na wamiliki wa maduka hayo mwaka
2015 kutoka mtaji wa sh milioni 40 hadi sh milioni 100 ambayo iliafikiwa kwa
kipindi cha miaka miwili.
No comments:
Post a Comment