Thursday, October 12, 2017

CRDB yachomoza kwa usalama duniani
Benki ya CRDB imetajwa miongoni mwa taasisi salama zaidi za fedha duniani, hivyo kuiweka Tanzania miongoni mwa nchi 11 kutoka Afrika zilizokidhi vigezo hivyo.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya Globa Finance ulihusisha nchi 106 na taasisi husika zikawekwa kwenye makundi ya benki 50 salama zaidi duniani, benki 50 za biashara salama zaidi duniani, benki 50 salama zaidi kutoka nchi zinazoibukia kiuchumi, benki salama zaidi ya Kiislamu na benki bora kwa kanda ya Afrika, Asia, Ulaya, Mashariki ya Mbali na Amerika.
Kukidhi vigezo na kuwemo kwenye orodha hiyo, Benki 1,000 kubwa zaidi zilifanyiwa tathmini kwa kuzingatia vigezo tofauti.
Mkurugenzi wa idara ya habari wa Global Finance, Joseph Giarraputo amesema kulikuwa na changamoto wakati wa kukamilisha mchakato huo na hasa kwa benki zenye matawi kwenye zaidi ya nchi moja na zinahudumia wateja wenye ofisi katika mataifa tofauti.
“Licha ya juhudi tulizozifanya kuzihuisha, kanuni za uendeshaji wa benki zimekuwa tofauti kwa kila nchi kutokana na changamoto zilizopo pamoja na rasilimali,” amesema Giarraputo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa amesema ushirikiano wa wafanyakazi wa taasisi hiyo ndiyo chachu ya mafanikio ndani na nje ya mipaka.
“Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa huduma bora kwa mteja. Usalama wa taarifa za wateja wetu ni kitu kinachopewa kipaumbele.
Hii ni kwa maeneo yote; mikopo, huduma za mtandaoni hata kwa simu za mkononi,” amesema Mwambapa.
Licha ya CRDB yenye thamani ya Sh5.49 trilioni, taasisi tatu kutoka kaskazini mwa Afrika nazo zimetajwa.
Hizi ni National Bank of Egypt (Misri), Attijariwafa Bank ya Morocco na Arab Tunisian Bank ya Tunisia.
Kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, kuna Banco Angolano de Investimentos ya Angola, Rawbank ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Standard Bank ya Afrika Kusini, GCB ya Ghana, Zenith ya Nigeria, Ecobank ya Togo na Stanbic ya Kenya.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KITUNDA DAR ES SALAAM YAFANA
Older Article
Tanga Cement yasaidia ujenzi wa nyumba za polisi zilizoungua mkoani Arusha
AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YATOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WATEJA WAKE KARIAKOO
kilole mzeeApr 13, 2025WADAU ZAIDI YA 500 KUSHIRIKI WIKI YA AZAKI 2025 MWEZI JULAI ARUSHA
Hassani MakeroApr 11, 2025JUBILEE HEALTH INSURANCE YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE,YAPEWA TUZO YA TSEA 2025
Hassani MakeroApr 08, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment