MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KITUNDA DAR ES SALAAM YAFANA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, October 12, 2017

MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KITUNDA DAR ES SALAAM YAFANA


Mkuu wa Shule ya Msingi Kitunda, Shani Mbunda (Kulia) akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi (hawapo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Laaso Group,Lawrence Sajilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, William Sanga, Mjumbe kamati ya shule, Rukia Mwatawala na Mwisho ni Mjumbe wa kamati ya shule Husein Shekwavi.


Mkurugenzi wa Laaso Group,Lawrence Sajilo (wapili kulia) akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitunda (hawapo pichani) katika hafla ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Mwisho kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Shani Mbunda na Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, William Sanga na Mjumbe wa wazazi,Huseni Shekwavi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya msingi Kitunda,William Sanga (Katikati) akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi (hawapo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Kitunda,Thobias Mushi (kulia) akimkabidhi risala Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, William Sanga.
Mkurugenzi wa Laaso Group,Lawrence Sajilo (kulia) akipeana mikono na Viongozi wa kamati ya shule ya Msingi Kitunda katika hafla ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wahitimu wa Darasa la saba wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa na walimu wao katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa hao iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.





Kikundi cha ngoma ya Asili cha Shule ya Msingi Kitunda kikitumbuiza katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.


Kikundi cha Mashairi cha shule ya msingi Kitunda kikimuimbia mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo (hayupo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.


Kikundi cha Kwaya cha shule ya msingi Kitunda kikimuimbia mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo (hayupo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.


Kikundi cha Wanamitindo cha wanafunzi wa darasa la nne wa shule ya msingi Kitunda kikimuonyesha mitindo mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo (hayupo pichani) katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.


Walimu wa Shule ya Msingi kitunda wakitumbuiza katika sherehe ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo (katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, William Sanga (kushoto) na Mkuu wa shule ya Msingi Kitunda Shani Mbunda wakikata keki katika hafla ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa shule ya Msingi Kitunda Shani Mbunda (kulia) akimlisha keki Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, William Sanga katika hafla ya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Darasa la saba iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Laaso Group, Lawrence Sajilo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages