Yumkini jaribio la mzee wa kiduku limeshtua sana
Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho
ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL
inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea
jimbo la Florida nchini Marekani.
Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi
yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy
Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na
wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya
kimarekani.
Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya
juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali
yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu
chake ni Sea, Air and Land.
Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na
majeshi mengine kama US Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala
wa Obama, ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho
kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama na ni
askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti ambayo
ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye makazi ya Osama.
Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua
haraka helicopter yao iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia
iliyotumika kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka.
Makomandoo wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani
Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal.
Na ikumbukwe kuwa Operation hii ilikuwa ikitazamwa
live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama alikuwa akifuatilia, kofia za
makomandoo hawa zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu
kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House. Mkakati huu
ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama Alfreda Frances Bikosky
ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi aliyebobea na pia ni komandoo
lakini si memba wa Navy Seal.
Bibi Alfreda anajulikana zaidi katika jeshi la
Marekani kama MALKIA WA MATESO. Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti
mitandao ya kijamii na google isisambaze picha za mama huyu hatari.
Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya
makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem
husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa
ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za
Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea),
Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama
walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa
Iran) na Foreign Internal Defence.
Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985
ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye
mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko
Virginia, Marekani.
Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA
kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa.
Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea
Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika
Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..
No comments:
Post a Comment