Mkurugenzi wa Baraza la
Dini na Amani Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Godda, akihutubia wakati
akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha
uhiishaji wa katiba mpya inayoendelea Hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar
es Salaam leo. Semina hiyo imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC).
Mkurugenzi wa Utetezi na
Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga
akizungumza kuhusu umuhimu wa semina hiyo kwa viongozi wa dini.
Meneja Mipango Msaidizi
wa (IRCPT), Rogers Fungo akizungumza katika
semina hiyo.
Mwenyekiti wa Taifa wa
Wanawake wa Baraza la Kiislam Tanzania (Bakwata), Shamim Khan (kulia),
akizungumza katika semina ya siku mbili ya viongozi wa dini kuhamasisha
uhiishaji wa Katiba mpya iliyofanyika Dar es Salaam leo. Semina hiyo
imeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Semina ikiendelea.
Wawakilishi kutoka
taasisi za dini wakiwa kwenye semina.
Viongozi wa dini wakiwa
kwenye semina.
BARAZA la Uongozi la Dini
na Amani Tanzania (IRCPT), limesema ipo
haja mchakato wa Katiba Inayopendekezwa
kufikia tamati kwa kuwa ina mambo ya msingi
kwa Watanzania.
Mkurugenzi wa Baraza
hilo, Mchungaji Thomas Godda amesema ni vema
viongozi wa dini wakatimiza wajibu wao kwa kuihamasisha Serikali imalize mchakato huo sanjari na kuhamasisha wananchi kusoma Katiba iliyopo ili kuwajengea uelewa mpana.
Ametoa kauli hiyo leo Dar
es Salaam kwenye semina ya siku mbili ya
kuhamasisha uhiishaji wa Katiba Mpya
kwa viongozi wa dini inayoendelea kwenye
Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es
Salaam ambayo imeandaliwa na Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Aliongeza kuwa viongozi
wa dini si wanaharakati bali ni watu
wanaotoa uamuzi wao kwa hekima huku
wakiaminiwa na wafuasi wao wakiwemo
viongozi wa serikali.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC,
Anna Henga amesema wameandaa semina
hiyo kwa ajili ya viongozi wa dini kwa
kuwa ni watu wenye ushawishi mkubwa
katika jamii ili kusukuma mchakato wa katiba mpya.
"Semina hii kwa
viongozi hawa wa dini ni maazimio yaliyofikiwa na
viongozi wakuu wa dini katika mkutano wa
kwanza tulioufanya ambapo
walitushauri tuendeshe semina kama hii kwa
viongozi wa dini kutoka sehemu mbalimbali
nchini ili kuwajengea uelewa mpana
wa kujua masuala ya Katiba,"
alisema Henga.
Mtoa mada katika Semina
hiyo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk.James Jese alisema kuna
umuhimu wa sheria iliyopitishwa kuelekea upigaji wa kura ya maoni ya katiba
mpya ifanyiwe marekebisho kwa kuwa imepitwa na wakati.
Mwenyekiti wa Taifa wa
Wanawake wa Baraza la Kiislam
Tanzania (Bakwata), Shamim Khan, amesema Rais
John Magufuli ameanza
kuliongoza taifa kwa weledi mkubwa hivyo ni
vema amalize pia mchakato wa kupata Katiba
Mpya.
No comments:
Post a Comment