Meneja wa Airtel Money kutoka
kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce akitoa elimu kwa mmoja wa watumiaji
wamitandano ya simu kwa namna Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana
kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa
kiwango cha gharama ile ile.
Mmoja wa watumiaji wa
simu akijaribu kuomba maelezo ya kuhusu huduma za kutuma na kupokea fedha
kwenda mitandao yeyote nchini kwa kiwango cha gharama ile ile
Makampuni ya simu za
mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda
mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile.
Kwenye muungano huo ambao
unaitwa Taifa Moja, makampuni matatu makubwa ya kutoa huduma za simu za mkononi
ya Tigo Tanzania, Airtel Tanzania na Zantel, wateja wanaweza kutuma pesa na
kupokea kutoka kwenye moja ya mitandao hiyo kwa gharama zile zile.
Hapo awali, kutuma pesa
au kupokea pesa kutoka mtandao tofauti mteja alikuwa akipokea ujumbe mfupi
ambao ilikuwa ni lazima apeleke kwa wakala wa mtandao ambao amepokea fedha
kutoka na ilikuwa izizidi siku saba tofauti na hapo fedha hiyo ilikuwa inarudi
kwa aliyetuma.
Kwa huduma hii, mteja
anapaswa kuchangia huduma ya kutuma pesa kutoka kwa menu ya kawaida, halafu
anachangua kutuma pesa kwenda mitando mingine.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutembelea watumiaji wa huduma za kutuma na
kupokea pesa, Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses
Alphonce alisema kupitia muungano wa Taifa Moja wameweza kuwafanya wateja
wapate njia rahisi ya kutuma na kupokea fedha.
Tunajua hapo zamani kuna
baadhi ya wateja walikuwa wanapata wakati mgumu linapokuja suala la kutuma na
kupokea fedha. Ilikuwa aidha upokee fedha kwa ujumbe mfupi au uwe na laini ya
simu zaidi ya moja. Ukipokea fedha kwa ujumbe na kwa bahati mbaya ukaufuta
ilikuwa inamaanisha fedha imepotea, alisema Alphonce.
Lakini vile vile si kila
mtu anayepokea fedha kupitia simu ya mkononi anahitataji kutoa. Wengine
wanataka kulipia huduma mbali mbali kupitia huduma ya simu kama kulipia maji,
kununua umeme au matumizi mengineyo. Kwa huduma hii mpya ya Taifa Moja imekuwa
ni njia rahisi kwa wateja wetu, aliongeza Alphonce
Kupitia huduma hii ya
kutuma pesa na kupokea kutoka mitandao yeyote itachangia kuongeza idadi ya watu
wanaotumia huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mkononi na pia
kuongeza faida kwa makampuni ya simu.
Hii ni mara ya kwanza
Tanzania kwa makampuni ya simu kuungana pamoja kwa huduma ya pamoja. Hata
hivyo, Taifa Moja sio huduma au mtandao mpya mbali ni njia ambayo imepewa
promosheni hii ya kutuma na kupokea fedha kutoka mtandao wowote.
Kwa upande wake, Mkuu wa
usambazaji mkoa wa Dar es Salaam kutoka kampuni ya Tigo Tanzania Lloyd Kaaya. Alisema
ni furaha kwao kuona kwamba wateja wa simu za mkononi kwa sasa hivi anaweza
kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote kwa gharama zile zile. Hii
inaamanisha matumizi wa kutuma pesa yataongeza na yatakuwa na manufaa kwa
upande wetu, alisema Kaaya.
No comments:
Post a Comment