Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu wanawake iliyoshiriki uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA)
katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa
michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji
baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu
20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu ya
Wavulana walioshiriki uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini
(Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya
uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa
kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na
wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akipiga penati kuashiria uzinduzi wa michezo ya
shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote
kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi
ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari
mkoani Dodoma.
Vifaa vya michezo.
Wanafunzi zaidi ya elfu 20 kutoka sekondari
wahudhuria
Kiu ya wanafunzi na wadau
wa michezi nchini kote kuhusiana na mashindano ya michezo na sanaa kwa shule za
sekondari nchini imekatwa rasmi siku ya jana, baada ya kufanyika uzinduzi wa
michuano hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Akifungua michuano hiyo
kwa mkoa wa Dodoma,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani
Jaffo alitoa pongezi kwa mchango wa kampuni ya Coca-Cola kuendeleza michezo
mashuleni, huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri kote nchini kuhakikisha
kuwa wanatenga viwanja vya michezo.
Vile vile, aliwaelekeza
maafisa elimu ngazi ya tarafa, kata, wilaya, mikoa pamoja na wakurugenzi wa
halmashauri nchini kuhakikisha kuwa vipindi vya michezo mashuleni vinaimarishwa
na kutumika kwa ajili ya shughuli za michezo na si kufundisha masomo mengine.
“Mtoto anayekosa
kushiriki michezo, hata akili yake huweza kufubaa. Michezo hujenga na
kuimarisha afyaya mwili na akili, upendo, ushirikiano na uzalendo”, alisema
Jaffo.
Aidha, aliongeza kuwa
wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na makaibu tawala wa mikoa
kuhakikisha kuwa kila shule ina viwanja vya michezo vyenye vipimo sahihi na
kusimamia sharia ya elimu inayotaka shule inaposajiliwa lazima kuwa na eneo la
viwanja vya michezo.
Ofisi ya Rais Tamisemi
haitowaangusha walimu wote wa michezo nchini katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, wakati
akihutubia hafla ya ufunguzi wa michuano hii, mwakilishi wa kampuni ya
Coca-Cola nchini, Pamela Lugenge aliwahakikishia washiriki kuwakampuni hiyo
itaendelea na dhamira yake ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini
kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbalimbali
ya michezo, ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa udhamini wa michuano ya
Copa-UMISSETA.
“Dhamira yetu katika
kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI ni endelevu, tukiwa
tumejidhatiti kuhakikisha tunaendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na
kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha nyanja ya michezo nchini
katika kiwango cha juu zaidi”, alisema Pamela.
Mbali na hayo, aliongeza
kuwa “Pamoja na kuwepo changamoto ndogondogo za hapa na pale, tutaendelea
kufanya kazi bega kwa bega na washirika wetu serikalini, pamoja na wadau
wengine wote wa michezo nchini, ili kwa pamoja tuweze kufanikisha na kusaidia
kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja
na mpira wa kikapu kwa vijana”.
Alimalizia kwa
kuwahakikishia wadau wa michezo nchini ya kwamba kwa mwaka huu kampuni ya
Coca-Cola imejipanga kwa dhati, kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya
ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa
timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu zinazoshiriki.
No comments:
Post a Comment