STAA DIAMOND PLATNUMZ AAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA TUKIO LA KUTEKWA KWA ROMA NA MONI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 7, 2017

STAA DIAMOND PLATNUMZ AAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA TUKIO LA KUTEKWA KWA ROMA NA MONI


Jumatano hii usiku katika mitandao ya kijamii zilianza kuzagaa taarifa za kuvamiwa kwa studio ya Tongwe Record na kukamatwa kwa rapper Roma Mkatoliki, Moni, producer wa Tongwe Record pamoja na wasanii wachanga wawili ambao majina hayo hayakupatikana mara moja pamoja na kuchukua baadhi ya vifaa vya studio hiyo.

Ikiwa bado haijajulikana walipo wasanii hao baadhi ya mastaa wameonekana kuguswa na tukio hilo kiasi kwamba wengi wao waliamua kuandika ujumbe mzito kupitia kurasa zao.


Usiku huu msanii Diamond Platnumz  kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonesha kusikitishwa na tukio hilo na kusema haoni nchi yetu inakoelekea badala yake ameamua kumuachia Mungu tu kwani yeye ndiye ajuaje tunakoelekea.


Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages