TEACHER’S Junction imetoa zawadi
kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa ujirani mwema kwa shule 19 binafsi.
Akizungumza katika hafla
hiyo Mwalimu Mstaafu na aliyekuwa Mmiliki wa Shule Binafsi, Athuman Ahmed
amesema kuwa mashindano upimaji wa wanafunzi kwa mtihani kutaongeza taaluma kwa
wanafunzi hao.
Ahmed amesema kuwa
Teacher’s Junction wamekuwa
kiungo kwa shule za sekta binafsi katika kuratibu masuala ya mitihani ya
ujirani mwema.
Amesema kuwa wanafunzi
walioshinda wameonesha uwezo wao na wakiendelea watakuwa ni hazina kwa taifa.
Afisa Miradi wa Teacher’s Junction, Salum Njama
amesema kuwa wataendelea kuwa na mitihani mbalimbali katika kuwaandaa wanafunzi
kitaaluma na sio ushindani kwa shule.
Njama amesema shule
zilizoshiriki katika mtihani huo 19 ambapo wanatarajia ushiriki wa shule nyingi
na kuweza kujua viwango vya taaluma kwa wanafunzi.
Amesema wamefanya katika
Mikoa ya Arusha , Mbeya pamoja na Mwanza na kila sehemu iliyofanyika wanafunzi
wameonyesha uwezo kitaaluma.
Mwalimu Mstaafu, Athuman Ahemed
akizungumza wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri mtihani wa
ujirani mwema ulioratibiwa na Teachers’s Junction kwa shule binafsi leo jijini
Dar es Salaam.
Afisa Miradi wa Teacher’s
Junction, Salumu Njama akizungumza juu ya uandaaji wa mtihani wa ujirani mwema
kwa shule binafsi wakati utoaji zawadi kwa wanafunzi iliofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Walimu, wanafunzi pamoja na
Teacher’s Junction wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla ya utoaji
zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment