Bunge limetangaza
kuwa, uchaguzi mdogo wa kupata wawakilishi wawili wa nafasi ya ubunge kwa Bunge
la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
sasa utafanyika Mei 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya
Katibu wa Bunge ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Thomas Kashilillah,
uteuzi wa wagombea utafanyika Mei 3.
Watakaopigiwa kura na
kuchaguliwa katika uchaguzi huo wataungana na wengine saba, sita wakiwa kutoka
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao
walishinda katika uchaguzi wa Aprili 4, mwaka huu.
Siku hiyo, Chadema licha
ya kuweka wagombea wao Lawrence Masha na Ezekiah Wenje, kura zao hazikutosha
hivyo kukosa sifa za kuchaguliwa.
No comments:
Post a Comment