Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon
Sirro amesema ombi la kufanya usafi katika mazingira ya ofisi za chama hicho,
lililowasilishwa na Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea Aprili 27 mjini Dodoma.
Amesema kutokana
na sababu za kiusalama pamoja na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea ndani ya
chama hicho, Mbunge huyo pamoja na wanachama wengine na wanashauriwa kila mmoja
kufanya usafi katika eneo lake analoishi au analofanyia kazi.
"Kitendo
hicho cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka katika maeneo mbalimbali kwa
kigezo cha kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na
atakayethubutu kujitokeza atachukuliwa hatua za kisheria," amesema Sirro.
Wakati huo
huo Kamanda Sirro amesema sakata la watu waliovamia mkutano wa iongozi wa CUF
wilaya ya Kinondoni na wanahabari hadi sasa wanawashikilia watu saba akiwemo
Mkurugenzi wa Mahusiano wa wa chama hicho, Abdul Kambaya.
Amesema
upelelezi wa kesi hiyo, umefanyika vizuri na tayari jalada limefikishwa kwa
Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya hatua zaidi ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Jeshi hilo
pia limewataka wananchi waliowahi kuibiwa magari yao kujitokeza katika Kituo
cha Polisi Mbezi ili kuangalia kutokana,na kupatikana kwa magari matano
yanayodaiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kitendo
cha wanachama wa CUF kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali kwa kigezo cha
kufanya usafi kinaweza kusababisha uvunjifu wa amani atakethubutu kujitokeza
atachukuliwa hatua za kisheria leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionesha madumu ya pombe haramu ya Gongo yaliyo
kamatwa katika oparesheni ya jeshi la polisi leo jijini Dar es Salaam.
Picha za magari yanayodaiwa kuibiwa
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment