WANADIASPORA KUFANYA MDAHALO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, April 8, 2017

WANADIASPORA KUFANYA MDAHALO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA UWEKEZAJI NCHINI


Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) pamoja na wanaoishi ndani ya nchi wanatarajia kufanya mdahalo Aprili 11, 2017 jijini Dar es Salaam, wa kujadili changamoto na fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini hasa biashara ya viwanda.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ikolo Investment LTD ambayo ndio muandaaji wa mdahalo huo, Maggid Mjengwa amesema katika mdahalo huo watajadili maendeleo ya nchi na namna ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaosukumwa na maendeleo ya viwanda.

“Mdahalo huo utashirikisha watu wapatao 300 kutoka katika makundi matatu ambayo ni watanzania wanaoishi na waliokuwa wakiishi ughaibuni na sasa wamerejea nyumbani pamoja na wanaoishi nyumbani ambao watajadili kufanikisha adhma ya serikali kuifanya nchi kuwa ya viwanda,” amesema.

Naye Katibu wa Kongamano hilo, Mwinyi Mwaka Khatib amesema kongamano hilo litasaidia wanaoishi ughaibuni kupata fursa ya kujadili namna ya kuanzisha viwanda pamoja na jinsi ya kuboresha bidhaa zinazozalishwa nchini ili zipate soko nje ya nchi.

“Katika harakati za kutambulisha bidhaa za Tanzania nje ya nchi kuna changamoto sababu hatujajipanga vizuri kutumia masoko ya nje kutokana na kushindwa kuzalisha bidhaa toshelezi zenye ubora. Mdahalo huo tutajadili namna ya kukidhi matakwa ya masoko ya nje ya nchi na kuanzisha viwanda nchini,” amesema.


Khatibu amesema mdahalo huo umekuja wakati muafaka kutokana kwamba, kwa sasa baadhi ya nchi zimeanza kutoa fedha za ruzuku kwa diaspora ili waje kuanzisha viwanda kwenye nchi wanazotoka.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages