WAZIRI MPANGO NA MWIJAGE KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, April 6, 2017

WAZIRI MPANGO NA MWIJAGE KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYABIASHARA


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabishara Aprili 11, 2017 mjini Dodoma kwa lengo la kusikiliza changamoto zao ili zitafutiwe ufumbuzi.
 Waziri wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage

Wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Wiki ya Kongamano la Biashara la Ufaransa na Tanzania Mwenyekiti wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema Rais John Magufuli amesikia malalamiko ya wafanyabiashara na kwamba mkutano huo utasaidia kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.

“Kusema kweli mazingira ya biashara Tanzania siyo mazuri mmeona malalamiko mengi kutoka sekta binafsi, wafanyabiashara wanalalamika kila mahali ukienda ni tatizo, kufuatia malalamiko hayo ya siku nyingi Rais ameyasikia na kuagiza mawaziri wake kuongea na sekta binafsi ili tutoe malalamiko yetu yote tunayoyaona katika uchumi huu unaongozwa na utawala wake,” amesema.

Hata hivyo, Simbeye ameeleza kusikitishwa kwake na mwitio mdogo wa Kampuni za Kitanzania katika kongamano hilo lililokutanisha kampuni arobaini kutoka nchini Ufaransa, na kusema kuwa zisizohudhuria zimekosa fursa nyingi za kibishara.

“Hizi kampuni zilizojitokeza hapa ni kubwa sana zinaweza kutoa fursa kwa kampuni za Tanzania kufanya sehemu ya shughuli wanazofanya zikafanyika Tanzania ila nilichosikitika sijaona mwamko wa kampuni za ndani kuja kushiriki katika kongamano hili, hili ni tatizo sababu wamekosa fursa labda hapo baadae tutawashauri waje waangalie fursa sababu zipo nyingi sana,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara nchini kutokata tamaa pia kuzitumia fursa zilizopo za kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Media Reginald Mengi


“Inatakiwa tujiamini kama wenzetu walivyothubutu, tumechoka kusema hatuwezi sababu umasikini sio tatizo bali ni changamoto na kwamba kila siku tuseme tunaweza,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages