MCHEZO wa ligi kuu
Vodacom Tanzania Bara baina ya Yanga na Mbeya City unatarajiwa kufanyika
kuanzia majira ya saa 12 badala ya saa 10 jioni kama ilivyozoeleka.
Akitoa taarifa hiyo
Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Yanga Salum Mkemi amesema kuwa
mchezo huo utachezwa majira ya saa 12 kutokana na uwanja kuwa na shughuli
zingine za michezo ambazo zitachelewa kumalizika.
Mkemi amesema kuwa
wanapenda kuwatangazia wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa soka
jijini Dar es salaam sanjari na mikoa ya karibu kwamba; mchezo wa Jumamosi kati
ya Yanga SC na Mbeya City utachezwa uwanja mkuu wa taifa usiku badala ya kuanza
saa 10:00 kama ilivyo ada.
Mchezo huo utaanza majira
ya saa 12:00 jioni kongwe kabisa nchini kucheza mchezo wake wa ligi kuu usiku
katika miaka ya hivi karibuni.
Maamuzi haya yamezingatia
matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu na hamu ya kuutazama
mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa mchezo wa riadha
itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo.
Mkemi amewaomba wanachama
na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao kwani ulinzi utakuwa
imara na thabiti.
No comments:
Post a Comment