BENKI ya NMB PLC
imeshinda tuzo mbili katika sherehe za utoaji wa tuzo wa benki bora duniani
zilizofanyika Jijini London, Uingereza. NMB Imetajwa kwa mara ya kwanza kuwa ni
Benki Bora ya Maendeleo Barani Afrika huku tuzo ya pili ikiwa ni Benki Bora
Tanzania 2017 hii ni mara ya Tano Mfululizo.
Kila Mwaka, Jarida la
Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za
kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote duniani kwa kuagalia benki bora na ya
kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takribani 100 duniani
kote. Tuzo hii huzitambua taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata
mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio
ya kifedha kila mwaka.
Jarida ya Euromoney
liliandika kuwa,“NMB siyo benki iliyo hai bali ni benki inayofanya kazi.
Maamuzi makubwa yanafanyika kwenye maeneo ya mtaji, biashara na watu yamekuwa
yanafanyika. Katika maboresho hayo, bado benki imeweza kutoa gawio zuri kwa
wanahisa kuliko taasisi yoyote ya fedha nchini.”
Mkurugenzi Mtendaji wa
NMB, Ineke Bussemaker alisema kuwa ubunifu katika huduma, tekinolojia na
uwekezaji katika fedha za kielektroniki kwa msaada wa mtandao mpana wa matawi
na ATM imechangia kuiboresha benki na kuifanya taasisi bora ya kifedha nchini.
“Kutatua changamoto za
jamii ya watu wasiotumia huduma za kibenki nchini inachukua uwekezaji, ubunifu
na uwezo wa kuwaleta wadau katika malipo na huduma zingine za kifedha,” alisema
bi Ineke
Bi Ineke alisema “kuwa ushindi wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na benki Bora Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania bali Afrika nzima.”
Bi Ineke alisema “kuwa ushindi wa tuzo mbili kwa mpigo za benki ya maendeleo Afrika na benki Bora Tanzania ni kielelezo tosha kuwa juhudi zetu zinaonekana situ Tanzania bali Afrika nzima.”
“Tunatoa shukrani zetu wa
wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya
makubwa kwa benk, “ alisema Bi Ineke na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi
yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku za mbeleni.
Akizungumza kwenye hafla,
Mhariri wa jarida la euromoney Bwana Clive Horwood alisema “mchuano wa kupata
tuzo mwaka huu ulikuwa wa ushindani sana katika taasisi zilizoshiriki na hivyo
kufanya uamuzi kuwa mgumu sana Benki zilizoshinda na kujipatia tuzo zetu
zimechukua hatua kubwa katika mipango yao ya kibenki. Mabenki huko miaka ya
mbele yatakuwa yanaangalia nini unafanya na pia nini ambacho hukifanyi. Mwaka
huu, benki zilizong’ara zimetafsiri kwa unaga ubaga ni wapi kwenye nguvu Zaidi
na kuzingatia maeneo hayo.”
No comments:
Post a Comment