Mkuu wa Masoko wa Benki ya DTB, Sylvester
Bahati (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni
ya Chakarika inayowasidia wateja wajasiriamali kuwaongezea ufanisi kwenye
biashara kwa kuwafungulia fursa mbalimbali kupitia akaunti zao. Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTB,
Viju Cherian na Mkuu wa Idara ya Huduma za kibenki wa benk hiyo, Kumar
Dandapani.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya DTB, Cherian (katikati),
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
Chakarika itakayowasidia wateja wajasiriamali kuwaongezea ufanisi kwenye
biashara kwa kuwafungulia fursa mbalimbali kupitia akaunti zao. Uzinduzi huo
ulifanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Masoko,
Sylevester Bahati na Mkuu wa Idara ya Huduma za kibenki wa benki hiyo, Kumar
Dandapani.
Benki ya
Diamond Trust Bank Tanzania leo hii imezindua “Chakarika Campaign” ambayo ni
kampeni mahususi iliyobuniwa katika kuwaongezea wajasiriamali ufanisi kwenye
biashara zao kwa kuwafungulia fursa mbali mbali kupitia Akaunti ya Biashara.
Kama neno “Chakarika” lisemavyo Akaunti hii ya Biashara imeundwa kwa
wajasiriamali wachakarikaji wenye malengo ya kukuza na kufanikiwa katika
biashara zao.
Kampeni ya
Chakarika inalenga kuhamasisha wajasiriliamali wanaochipukia kuacha kutumia
akaunti zao binafsi katika kufanya miamala ya kibiashara na kufungua Akaunti
hiyo ya Biashara. DTB Tanzania imeboresha Akaunti ya Biashara kwa kupunguza
kiwango cha kufungulia akaunti hiyo hadi TSHs 50,000 na kupunguza makato ya
kila mwezi mpaka TSHs 12,000 kwa mwezi. Kampeni hiyo pia itatoa fursa kwa kila
anayefungua Akaunti ya Biashara kushinda zawadi mahususi katika kipindi kizima
cha Kampeni hiyo.
Ndani ya
miaka 9, DTB Tanzania imeweza kupanda katika nafasi ya 5 kutoka nafasi ya kumi
kwa ukubwa wa Amana za Wateja kati ya mabenki zaidi ya 50 nchini. Ndani ya muda
huu DTB Tanzania pia imefanikiwa kukuza mtandao wao wa matawi kutoka matawi 6
tu mpaka matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam.
Fursa kwa
wajasiriamali zinazopatikana kupitia kampeni hii ni pamoja na fursa ya kukuza
mitaji, uhifadhi wa kumbukumbu za biashara pamoja na uwezo wa kufanya miamala
ya kibashara kwa wakati. Akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Kampeni
hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa DTB Tanzania, Ndugu Viju Cherian alisema,
“Mafanikio makubwa ya DTB Tanzania ndani ya miaka 9
iliyopita yametokana na jitihada za watendaji chipukizi walio makinikatika
kutoa huduma.” DTB inajivunia kuwa watendaji ambao wamepitia mafunzo maalum ya
kunoa ujuzi katika maswala ya kibenki na ya huduma kwa wateja.
Ndugu
Cherian aliongeza kwa kusema, “Kutoa huduma bora kwa haraka ni tamaduni
yetuhivyo kuwapa wateja wetu muda wa kufanya mambo mengine yenye tija zaidi
yakiwemo kukuza biashara zao na kutumia muda na ndugu na marafiki.” Pamoja na
matawi 28 yaliyotapakaa nchi nzima, DTB Tanzania pia inatoa huduma kwa njia
mbadala kupitia Internet Banking, Mobile Banking pamoja na mtandao wa mashine
za ATM.
“Dhamira
yetu kubwa kama benki ni kutoa huduma zilizo kamilika, huduma zinazotosheleza
mahitaji ya kila mteja bila kujali umri, jinsia au hali yao ya kifedha. Sisi ni
Benki ya kila Mtanzania na hii inaonekana dhahiri katika huduma tunazotoa.
Kupitia Kampeni ya Chakarika, ningependa kuwakaribisha wajasiriamali wote,
waliobobea na wanaochipukia kutembelea matawi yetu na kufungua akaunti nasi.”
aliongeza Ndugu Cheria.
DTB
Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam
kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala,
Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa
Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo)
jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani
City. Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na
tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara,
Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.
DTB
Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha
shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini
Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga
Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development –
AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development
Network -AKDN)
No comments:
Post a Comment