Hatimaye kampeni ya Magift inayofanywa na kampuni ya Yas Tanzania ,kupitia kitengo cha Mixx by Yas imeweza kuwazawadia, wateja na washindi wake wa mkoa wa mtwara zawadi mbalimbali, ikiwemo fedha na gari Moja.
Akizungumza mara baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya Mixx by Yas, Zena Ponera ambaye ni mkazi wa manispaa ya Mikindani mjini mtwara ameelezea MIKINDANI Siri ya ushindi huo, ambapo mbali na mambo mengine amesishukuru Yas kwa kufanikisha kuchezesha Droo za Magift ya KUGIFT 2024-25.
Kwa upande wake Meneja wa Yas Kanda ya Mtwara, Eric Munuku,ameelezea namna kampeni hiyo ilivyoweza kuwanufaisha watanzania wengi ambao wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha magari na zawadi za simu za mkononi Kutoka Yas na Mixx by Yas.
Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya Yas Tanzania kwa kipindi cha miezi miwili na nusu iliyopita iliendesha kampeni hiyo nchi ambapo jumla ya washindi Zaidi 300 walifanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali Kutoka Kampuni ya Yas Tanzania.
No comments:
Post a Comment