Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage (kushoto),
akizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)
Mh. Almas Maige (kulia), huku Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka
akisikiliza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam
juni 29, 2017.
Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto)
akilakiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Almas
Maige (kushoto), na Mratibu wa Mradi wa Mwanamke wa Wakati Ujao, Lilian
Machera (kulia) alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama
hicho, Dar es Salaam juni 29, 2017.
Mwenyekiti
Mpya wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mama Jayne Nyimbo (wa
pili kushoto), akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo wakati
wa Mkutano Mkuuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana. Wengine
kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka, aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Almas Maige na Makamu Mwenyekiti mpya, Felix
Kagisa.
Mkurugenzi
Mtendaji
wa Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa chama hicho
wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea.
Baadhi
ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi
ya washiriki katika mkutano huo wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Charles
Mwijage ambaye alisema serikali itaendela kujenga mazingira mazuri ya utoaji
vibali vya uwekezaji ili kuweza kufikia ajenda yake ya kuimarisha uchumi wa
viwanda.
Aliyekuwa
Mwenyekiti Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mhe. Almas Maige
akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika pamoja na mkutano kujadili
masuala mbali mbali kuhusu ajira na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment