Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.
Katika
mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa
kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake
inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye
alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Nafasi
ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa
Polisi wa Mkoa wa Mara.
Uhamisho huo
ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika
kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Imetolewa
na:
Barnabus
D. Mwakalukwa - ACP
Msemaji
wa Jeshi la Polisi.
Makao
Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment