Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya
kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya
Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (mwenye jembe), akipiga tuta la kupandia
mbogamboga katika eneo la kijiji cha watoto yatima cha Malaika, katika hafla
ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti ya matunda na mbogamboga na
kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula ikiwa ni sehemu ya
shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani jumamosi
iliyopita.
Meneja Uendeshaji
wa kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari
na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Jayne
Nyimbo (katikati), akipanda miti pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa katika
kituo cha watoto yatima cha Malaika Village, katika hafla ambayo wafanyakazi wa
kampuni hiyo walipanda miti ya matunda na mboga mboga na kisha kukabidhi msaada
wa aina mbalimbali za vyakula ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo
hicho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya
kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya
Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (kulia), akikabidhi msaada wa aina
mbalimbali za vyakula kwa Meneja wa kijiji cha Malaika, James Kalinga
(kushoto), katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanykazi wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia kuandaa shamba
kwa ajili ya upandaji wa mbogamboga katika hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Cartrack, Albert Mdemu (katikati),
akipanda miti pamoja na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha watoto yatima
cha Malaika, kilichopo Mkuranga, Pwani
juzi.
Baadhi ya
wafanyakazi wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia kuandaa shamba kabla hawajapanda
mbogamboga ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii.
Watoto
wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakifurahi pamoja na wafanyakazi wa
Cartrack waliotembelea katika makazi yao na kuwasaidia katika upandaji miti ya
matunda na mbogamboga.
Watoto wanaolelewa katika
Kijiji cha Malaika wakila chakula huku wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Cartrack Tanzania, Anna Nyimbo (kulia nyuma), walipowatembelea katika makazi
yao na kuwasaidia katika upandaji miti ya matunda na mbogamboga.
Meneja Uendeshaji wa Cartrack Tanzania, Bi. Jayne Nyimbo (katikati)
akiwa na baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika.
Watoto
wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakiwasindikiza baadhi ya wafanyakazi wa
Cartrack baada ya kuhitimisha ziara yao kituoni hapo. Mkurugenzi Mtendaji wa
Cartrack, Bi. Anna Nyimbo alisema miti ya matunda na mbogamboga walizopanda
zitawasaidia watoto hao katika mahitaji
ya kila siku hivyo kupunguza utegemezi wa misadaa. (All photo vby Peter
Mgongo)
No comments:
Post a Comment