Saturday, August 12, 2017

KARIA RAIS MPYA TFF, WAMBURA AWA MAKAMU
Na Mwandishi Wetu, DODOMA
WALLACE KARIA ndiye Rais mpya wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika leo
kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la St. Gasper mjini Dodoma.
Karia amewashinda mchezaji wa zamani wa timu ya
taifa, Ally Mayay, Katibu wa zamani wa shirikisho hilo, Frederick Mwakalebela,
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Wakili Imani Madega, Mwandishi wa
Habari za Michezo wa zamani, Shija Richard na Katibu wa klabu ya Mbeya City,
Emmanuel Kimbe.
Michael Richard Wambura ameshinda nafasi ya
Umakamu wa Rais akiwaangusha Mwenyekiti wa FA ya Dodoma, Mulamu Nghambi,
mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na
Stephen Mwakibolwa.
Wallace Karia ndiye Rais mpya wa TFF, baada ya kuibuka
kidedea katika uchaguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la
St. Gasper mjini Dodoma.
Baada ya matokeo hayo, washindi wote wa
waliapishwa kwa agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk.
Harrison Mwakyembe.
Ikumbukwe aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi
ameshindwa kurudi kutetea nafasi yake baada ya kuwekwa rumande tangu Juni 29, mwaka
huu kwa pamoja na Katibu wake, Selestine Mwesigwa na Isinde Isawafo Mwanga kwa
tuhuma za ubadhirifu.
Watatu hao walipelekwa rumande Juni 29 baada ya
kusomewa mashitaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF
iliyopo katika banki ya Stanbic, Dar es Salaam.
Katika mashitaka hayo, 25 yanakwenda moja kwa
moja kwa Rais wa shirikisho hilo, Malinzi akidaiwa kughushi michakato
mbalimbali ya kifedha, huku matatu yakiwahusu wote na Katibu wake na Mhasibu
wake Nsiande Isawafo Mwanga.
Malinzi aliingia madarakani TFF Oktoba mwaka
2013 baada ya kupata kura 72 kati ya 126 zilizopigwa akimshinda aliyekuwa
mpinzani wake wa karibu, Athumani Nyamlani, lakini baada ya kesi hiyo kuanza
kuunguruma na kuwekwa rumande.
Kamati ya Utendaji ya TFF ilikutana na kumteua
Makamu wake, Wallace Karia kukaimu Urais wa shirikisho hilo.
Tags
# MICHEZO
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
MAGAZETI YA JUMATATU LEO AGOSTI 14, 2017
Older Article
MKURUGENZI WA AL MUNTAZIR SEMINARY AINUA ELIMU NCHINI
NBC Kutumia Mchezo wa Gofu Kuchochea Ushirikiano wa Kibiashara
Hassani MakeroMar 24, 2025TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
Hassani MakeroMar 08, 2025WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA KUSHIRIKI MBIO ZA YAS KILI INTANATION HALF MARATHON
kilole mzeeFeb 15, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment