Mkurugenzi wa Shule zote za Al
Muntazir Mohamood Ladak akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mdahalo
unaofanyika katika Shule yake iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakishiriki kikamilifu
katika mdahalo unaendelea kufanyika jijini Dar es Salaam katika shule ya
seminary ya AL Muntazir.
Baadhi wa wanafunzi wakikiliza kwa
umakini mada iliyokuwa ikichangiwa na wanafunzi katika mdahalo (Bedate).
Mmoja wa washiriki katika mdahalo
huo akiongea jambo mbele ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali kutoka ndani
na nje ya nchi.
Zaidi Wanafunzi 250
wa Sekondari kutoka nchi mblimbali barani Afrika weanaza Mashindano ya mdahalo
(Debete) yanayofanyika katika shule ya Al Muntazir Seminary iliyopo jijini Dar
es Salaam.
Mashindano hayo
yenye lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi jinsi ya kijieleza, kujiamini jambo
ambalo linaweza kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Shule zote za Al -Muntazir Islamic Mahmood
Ladak, amesema kuwa katika mashindano hayo kuna jumla ya shule 15 kutoka
Tanzania, huku nyingine zikitoka nchini Zimbambwe, Afrika ya Kusini pamoja na
Uganda.
Ladak amesema kuwa
kwa lengo la mashindano hayo ni kuwakutanisha wanafunzi wa kitanzania na wezao
kutoka kutoka nchi mbalimbali ili kubadilishana mawazo ya kielimu waliojifunza
darasani.
Amesema kuwa
mashindano hayo yanajulikana kwa jina ‘Mwalimu Nyerere School Inventation
Debete Championship’ yanayotarajiwa kumalizika Agosti 13 mwaka huu.
Amefafanua kuwa
miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika mdahalo huo ni pamoja na mfumo wa
kimataifa (National system) pamoja na matukio mbalimbali.
“Kuna mada
mbalimbali ambazo wanajadili ikiwemo na mada zinazohusu masomo kwani zinawapa
fursa wanafunzi kubadilishana ufahamu wa kimasomo” amesema Ladak.
Naye Mratibu wa
Taasisi inayojiusisha na masuala ya mdahalo (Debete) Dominic Mwakifulele,
amesema kuwa katika kufanikisha mdahalo huu walitumia utaratibu wa wa
kuwaandikisha shule ambazo zitashiriki (Process registration) kupitia kampeni
ya mitando ya kijamii, pamoja na vyombo vya habari.
Hata hivyo baadhi ya
wanafuzi kutoka shule mbalimbali wameonekana kufurai mdahalo huo ambao
unawajenga kiakili.
Mduduzi Mhlanga ni
mwanafunzi kutoka Shule ya St John Collage nchini Zimbabwe amesema kuwa
mashindano hayo ni mazuri kwani yanawajenga katika kujieleza na kujiamini
katika masomo yao.
Naye mwanafuzi Hawa
kutoka Shule ya Al Muntazir Islamic Seminary ameushukuru uongozi wa shule
anayosoma kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yameonekana ni rafiki kwa
wanafunzi.
Bill Bob Luomba
ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Al-Muntazir amesema kuwa ni fursa kwao katika
kuhakikisha wanafanya vizuri katika mdahalohuo.
Amesema kuwa mada
mbalimbali zinaendelea kujadiliwa katika shule anayosoma ambayo imeonekana
kiwapatia wanafunzi wake fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo ili waendelee
kufanya vizuri.
Miongoni mwa shule
zinazoshiriki kutoka Tanzania ni pamoja na Al Muntazir Islamic Seminary ambao
ni miongoni mwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo yanafanyika
nchini Tanzania mara ya pili.
Washiriki wa
mashindano hayo ni shule za watu binafsi (Private) kutokana na kile
kinachodaiwa wanafunzi wengi wa shule za Serikali wamekuwa wakikabiliwa na hofu
ya kutoongeza kiingireza.
No comments:
Post a Comment