RC MAKONDA APOKEA MSAADA WA KOMPYUTA 200 KUTOKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO NIDA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, August 2, 2017

RC MAKONDA APOKEA MSAADA WA KOMPYUTA 200 KUTOKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO NIDA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Paul Makonda wa pili (kushoto), akipokea msaa wa Kompyuta za kisasa 200 zenye dhamani ya shilingi milioni 210 za kitanzania kutoka kwa maofisa wa kiwanda cha kutengenezea nguo (NIDA), kwaajili ya matumizi ya jeshi la polisi kuanza mfumo wa uratibu wa Taarifa za uharifu Mkoa wa Dar es Salaam, makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Samaam Paul Makonda, akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Samaam leo. katika hafla ya kupokea msaada wa kompyuta kutoka katika kampuni ya kutengeneza nguo NIDA.
Mkurugenzi Mtendaji, wa kiwanda cha kutengeneza nguo (NIDA), Mohamed Hamza, akiongea na waandishi wa habari ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa jijini Dar es Samaam Paul Makonda leo. alipokwenda kukabidhi msaada wa Kompyuta 200.
Paul Makonda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Jumla ya kompyuta za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd.

Mhe. Makonda  amesema  Kompyuta hizo atazigawa katikaVituo vya Polisi  20 kwaajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zitakazo ripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.

Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo chochote cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.

Makonda alisema mwonekano mpya wa Jeshi letu la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi”

Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.

Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza  uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda nae atapata taarifa.

Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara Mhalifu ambae  matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.

“Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi nan a utarahisisha utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages