Waziri
wa viwanda na uwekezaji Charles Mwijage akiwa pamoja na Viongozi kutoka
Danube pamoja na Balozi wa Duka hilo la Danube Zarina Hassan kwa pamoja
wakikagua baadhi ya bidhaa ambazo hupatkana kwa wingi katika Duka hilo
baada ya kuzindua duka hilo jipya lililopo mliman city.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya GSM na washirika wake Danube kwa kutoa fursa za ajira kwa watanzania zaidi ya watu 50.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage ameipongeza kampuni ya GSM na washirika wake Danube kwa kutoa fursa za ajira kwa watanzania zaidi ya watu 50.
Waziri
Mwijage amesema hayo katika uzinduzi wa duka hilo jipya la samani,
Danube
Mlimani City na kusema kuwa ni fursa nyingine pia kwa watanzania kwani
samani ambazo zitatumika kutengenezea samani hizo zitakuwa zikitoka
hapahapa nchini pia kuongeza soko la ajira kwa vijana wakitanzania.
Naye
Balozi wa Danube Zarina Hassan amesema kuwa anafuraha kubwa sana
kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa balozi wa duka hilo pia anawasihi wananchi
kujitokeza kwa wingi kujipatia huduma katika duka hilo kwani hata
gharama zake ni za kawaida ambazo hata mwenyekipato cha kawaida anaweza
kumudu.
Purukushani
zilitawala nje ya duka hilo wakati kila mmoja akijaribu kumsukuma
mwenzake ili aweze kumuona Zari ambae pia ni balozo wa duka hilo
aliyekuwa amekaa katika makochi baada ya uzinduzi wa duka hilo.
Watu
walivutiwa kumuona mwanamke huyo kutokana na hivi karibuni kupamba
vichwa vya habari baada ya mpenzi wake kukiri kuzaa na mwanamitindo
Hamisa Mobetto.
Ujio wa Zari nchini amekuwa na mvuto kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakilinganisha matukio katika maisha ya Zari na Hamisa.
Ujio wa Zari nchini amekuwa na mvuto kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakilinganisha matukio katika maisha ya Zari na Hamisa.
baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka hilo
No comments:
Post a Comment