Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka
madiwani wasio na shughuli ya kuwaingizia pesa binafsi kujiuzulu, kwani
serikali yake haiwezi kuwaongezea posho wanayohitaji.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT)
uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam, na kusema
kwamba Madiwani hao walifahamu masharti ya kugombea nafasi hiyo, hivyo
kama wameshindwa kuyatimiza ni vyema wakajiuzulu.
“Ndio
maana diwani masharti tunapojaza fomu tunaambiwa lazima uwe na kazi
maalum inayokupa kipato, sasa kama wapo madiwani waliojaza hiyo nafasi
na hawana kazi ya kuwapa kipato, wajiuzulu udiwani”, amesema Rais
Magufuli.
Leo
katika hotuba iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli ikisomwa na Mwenyekiti
wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) Bwana Gulam Mkadam, waliomba
kuongezewa posho za madiwani, kutoka Tsh. 300,000 hadi Tsh. 800,000
jambo ambalo Rais amelipinga.
No comments:
Post a Comment