Mstahiki Meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Shinyanga, Gulamhafeez Abubakar Mukadam (wa pili kulia), akipokea msaada wa mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Meneja Kiwanda wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Mhandisi Ben Lema, iliyotolewa na kampuni hiyo kuchangia ukarabati wa miundombinu katika shule za mkoani Shinyanga. Hafla ya makabidhiano ya saruji hiyo yenye thamani ya shs 6,047,500 ilifanyika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga hivi karibuni. Katikati yao ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TCPLC.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Shinyanga, Gulamhafeez Abubakar Mukadam (wa sita kushoto), akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Meneja Kiwanda wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wanne kushoto), iliyotolewa na kampuni hiyo kuchangia ukarabati wa miundombinu katika shule za Mkoani wa Shinyanga. Hafla ya makabidhiano ya saruji hiyo yenye thamani ya shs 6,047,500 ilifanyika eneo la kiwanda, Pongwe, Tanga mwishoni mwa wiki. Wa tano kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TCPLC.
Ofisa Mawasiliano wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kushoto), akizungumza kabla ya tukio la makabidhiano ya msaada wa saruji kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Halmashauri ya Shinyanga, Gulamhafeez Abubakar Mukadam (wa pili kulia).
Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Mtanga Noor (kushoto), akisalimiana na Mstahiki Meya Gulamhafeez Abubakar Mukadam wakati akiwasili katika kiwanda cha saruji cha kampuni hiyo, Pongwe nje kidogo ya mji wa Tanga kupokea msaada huo. Katikati ni Meneja Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema.
Meneja Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema (kushoto), akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Tanga, Radhiya Msuya huku Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinynga, Gulamhafeez Abubakar Mukadam (katikati), akiangalia katika hafla hiyo ambayo Tanga Cement ilikabidhi msaada wa mifuko 500 ya saruji kusaidia shughuli za ukarabati wa miundombinu katika shule za manispaa ya Shinyanga. Kulia kabisa ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya nje wa kampuni hiyo, Mtanga Noor.
No comments:
Post a Comment