Wabunge 8 na madiwani 2 wa CUF waliofukuzwa, Warudishiwa Uanachama hadi kesi ya Msingi itakapotolewa Uamuzi na Mahakama - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, November 12, 2017

Wabunge 8 na madiwani 2 wa CUF waliofukuzwa, Warudishiwa Uanachama hadi kesi ya Msingi itakapotolewa Uamuzi na Mahakama


Kuna taarifa kwamba wabunge wa viti maalumu waliofutiwa uanachama wa CUF na Lipumba wameshinda pingamizi lao mahakamani na mahakama imeamuru warejeshewe uanachama wao na ubunge.Kwa sababu hiyo wabunge wa Lipumba itabidi wakatafute kazi nyingine ya kufanya.

======

WABUNGE CUF WASHINDA MAOMBI YA ZUIO DHIDI YA LIPUMBA NA WENZAKE KATIKA KESI YA KUWAVUA UANACHAMA:

TAREHE 13/11/2017 WAJUMBE WA BODI YA WADHAMINI FEKI YA LIPUMBA WAITWA MAHAKAMA KUU KUJIELEZA MBELE YA MHE. JAJI NDYANSOBERA.

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF-CHAMA CHA WANANCHI)

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

LEO IJUMAA TAREHE 10 NOVEMBA, 2017 Mbele ya MHESHIMIWA JAJI LUGANO MWANDAMBO , MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi (Ruling) juu ya Maombi ya Zuio (Temporary Injunction) dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri dogo la madai [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2 kutoka Mahakama Kuu ni kama ifuatavyo;

1. Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

2. Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF [Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote KUJADILI juu ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

3. Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF [WAPELEKA MAOMBI -APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI YAO ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO YALIYOWASILISHWA MBELE YAKE.

4. Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliwekwa na Lipumba na Wenzake katika shauri hili.

Haya ndio maamuzi ya msingi yaliyotolewa Leo MAHAKAMA KUU. Maamuzi haya tafsiri yake ni kwamba kile alichokifanya SPIKA WA BUNGE Job Ndugai ni BATILI, NA WABUNGE 8 NA DIWANI 1 WA MANISPAA YA TEMEKE WALIOAPISHWA NI BATILI KWA KUWA WAHUSIKA WOTE BADO NI WANACHAMA HALALI WA THE CIVIC UNITED FRONT[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]. NI KWA MSINGI NI HUO Hatua na taratibu za kisheria zitachukuliwa kuhakikisha kuwa HAKI INAREJESHWA KWA WENYE KUSTAHIKI NAYO NA WABUNGE WA LIPUMBA WATATOKA BUNGENI.

Aidha, Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za Mwanasheria wa Manispaa wa Ubungo na Temeke juu ya utaratibu uliotumika Manispaa zao kufikishwa Mahakamani hapo kuwa haukufuata taratibu za kisheria na kwamba Mahakama haina Mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuchunguza Maamuzi yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi [NEC] kwa Mujibu wa Katiba na Sheria.

MAHAKAMA KUU IMEFUNGUA MLANGO WA KUSHUGHULIKIA Shauri la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Lililopangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 13/2/2017 kati ya Wabunge wetu 8 ambao ndio WADAI [APPLICANTS]

1. MIZA BAKARI HAJI
2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]
3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]
4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]
5. RIZIKI SHAHRI NG'WARI [MBUNGE]
6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]
7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]
8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]
9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA TEMEKE.
10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA UBUNGO.

DHIDI YA WADAIWA [RESPONDENTS]

1) BODI YA WADHAMINI -CUF,
2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,
3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,
4) MKURUGENZI TUME-NEC,
5) KATIBU WA BUNGE,
6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE
7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO
8) RUKIA AHMED KASSIM,
9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,
10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,
11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,
12) HINDU HAMIS MWENDA,
13) SONIA JUMAA MAGOGO,
14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,
15) NURU AWADH BAFADHILI

HOJA ZA WABUNGE WETU :

1. Wabunge na Madiwani Wetu walikuwa wanadai HAKI YA UANACHAMA WAO ambayo tayari leo imerejeshwa kwao.

2. Wanahoji jinsi mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya kuwavua uanachama kwa mujibu wa Katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro uliopandikizwa na Vyombo vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya siasa nchinji unaoendelea.

3. Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa rasmi za tuhuma zao kwa maandishi, siku na tarehe ya kikao hicho, kupata nafasi ya kujitetea, huku ikizingatia kuwa si wote wanaoishi Dar es Salaam, kulikofanyika kikao cha maamuzi.

4. Uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha vyakutosha.

5. Kutokupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CUF na vikao kuendeshwa kwa speed ya mwendokasi-‘DART'

6. Maamuzi hayakuzingatia haki za kikatiba za mwanachama ikiwemo haki ya kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya Chama.

7. Je Vyombo vilivyowachukulia hatua za kinidhamu vina uhalali wa Kikatiba ndani ya CUF? Hayana mengine mengi ndiyo yanayohojiwa Mahakamani katika shauri hili la msingi.

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Mawakili wetu Wasomi Peter Kibatara na Omary Msemo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kulisimamia suala hili kwa weledi mkubwa. Tunawapongeza Viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali za Chama, Wanachama, Madiwani na Wabunge wote waliokuwa pamoja na CHAMA NA AMBAO HAWAKUKUBALI KUYUMBA WALA KUYUMBISHWA kwa kufanikisha na kusimamia mapambano haya ya kisheria. Tunaamini na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwamba HAKI NA USHINDI VIPO KARIBU KUPATIKANA.

JAJI NDYASOBERA ATOA AMRI YA KUITWA WAJUMBE BODI YA RITA:

Katika hatua nyingine ya mapambano ya kisheria Jumatatu Tarehe 13/11/2017 Mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini FEKI' ya Lipumba wameitwa Mahakama Kuu kwenda kujieleza MMOJA MMOJA juu ya uhalali wao.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa leo Tarehe 05/10/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages