QNET YATATUA CHANGOMOTO ZA WATOTO YATIMA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, December 20, 2017

QNET YATATUA CHANGOMOTO ZA WATOTO YATIMA


Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki akikabidhi misaada mbalimbali ikiwepo vyakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo wengine pichani ni baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Mwakilishi wa QNET Tanzania, Benjamin Mariki (kulia) akikabidhi mashine ya  kusafishia  maji ya kunywa (water purifier) pamoja na mahitaji mengine ya kibinadamu  kwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Khayraat Orphans Centre kilichopo Kigogo Kati, Bi. Khadija Hussein, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.

Moja kati ya taasisi inayokua kwa kasi sana Tanzania ya masoko ya mtandao QNET, leo imetoa msaada wa mashine yenye mfumo wa kusafisha maji ya Water purifier na chakula chenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 kwa kituo cha watoto yatima cha Khayraat jijini Dar es salaam.

Msaada wa QNET ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo za kuwajibika katika jamii, ambazo zimeelekezwa katika kutoa msaada wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa zaidi ya watoto 500 wenye uhitaji katika kituo cha kulelea watoto yatima na kuwapatia chakula kwaajili ya kuwawezesha kufurahia sikukuu za krimasi katika kipindi hiki cha sikukuu kama watoto wengine.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa QNET Tanzania Benjamin Mariki, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja ina sera bora ya uwajibikaji kwa jamii ambayo inatafuta kutoa kwa jamii inayoihudumia.

“Katika kampuni ya QNET, tunaamini kuwa zaidi ya kusambaza bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kwa wateja wetu, tuna jukumu la kusaidia serikali na wadau wengine katika kutekeleza shughuli ambazo zina athari nzuri kwa jamii, hasa miongoni mwa wanajamii wenye uwezo mdogo,” alisema Mariki.

Mariki alisema kuwa msaada uliotolewa kwaajili ya kituo ni pamoja na ufungaji wa mashine ya kusafishia maji, kilo 100 za Mchele, kilo 100 za maharage, kilo 100 za unga, lita 60 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za sukari, kilo 100 za sabuni ya kufulia pamoja na biskuti, pipi na juisi.

Akipokea msaada huo, Mwasisi wa kituo cha Khayraat Orphans Centre, Bi Khadija Khussein aliishukuru kampuni ya QNET kwa kutoa msaada akisema kuwa msaada huo utawasaidia kwa kiwango kikubwa watoto walioko kituoni.

“Tunashukuru kwa msaada huo tukiwa tunatambua kuwa mashine ya kusafishia maji ya water purifier itasaidia katika kurahisisha upatikanaji wa maji safi na salama kwaajili ya watoto, hivyo kutoa uhakika wa afya kwa watoto kwa kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa maji kama vile typhoid na Kipindupindu wakati vyakula vitawapa watoto nafasi ya kufurahia sikukuu ya krimasi na mwaka mpya”. Alibainisha Bi Khussein.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages