AIRTEL SASA KUONGEZA KIWANGO CHA GB MARA MBILI KWA BEI ILEILE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, December 19, 2017

AIRTEL SASA KUONGEZA KIWANGO CHA GB MARA MBILI KWA BEI ILEILE

Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga akitoa Maelezo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa blog mbalimbali kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ 

Airtel yafanyia kazi changamoto za watanzania.
Ikiwa na lengo lakurahisisha mawasiliano kwa  watanzania kote nchini.

Moja ya makampuni ya mawasiliano yanayokuwa kwa kasi zaidi nchini, Airtel imesema kwamba itaendelea  kutoa huduma zake  kwa wateja wake kwa ubora zaidi na kwa bei nafuu 
Akiongea na waandishi  wa habari za mitandaoni (Blogers) Meneja  Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando  alisema kwamba maboresho ya vifurushi vya intaneti vimefanywa ili kukidhi hali ya kiuchumi na mahitaji ya  watanzania.

Tumeamua kuongeza kiwango cha Baadhi ya GB  mara mbili ya kile tulichokuwa tukitoa mwanzo kwa bei  ile ile ili kumuwezesha  mtanzania kufurahia thamani ya pesa yake alisema Mmbando.

aliongeza kwakusema kwamba kwa mara ya kwanza  kampuni hiyo imekuja na  kifurushi cha shilingi mia mbili (200)Kifurushi  hiki kinamwezesha mteja wetu kupata  MB 40.

kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Anethy Muga, alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bando za gharama nafuu na kabambe za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages