RC MAKONDA AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA KAMPUNI YA DAR COACH LTD - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Tuesday, January 16, 2018

demo-image

RC MAKONDA AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA KAMPUNI YA DAR COACH LTD

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya Ziara katika kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza,  ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.


Akizungumza mara baadaya kutembelea Kampuni inayofanya Ukarabati wa magari hayo Makonda amesema kuwa zoezi la Ukarabati  hayo litasaidia kuboresha mazingira ya kazi kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuwa kazi ya Ulinzi na Usalama ni wa Raia na linahitaji mazingira rafiki ya kazi.

Aidha  Makonda amedhibitisha kulidhishwa na kasi ya ukarabati wa mabasi hayo ambapo amekishukuru kiwanda cha Dar Coach Ltd kwa uzalendo wa kujitolea kukarabati Magari hayo ili kuongeza ufanisi katika vyombo vya ulinzi na usalama.

"Kama mnavyokumbuka Magari haya ni yale yaliyokuwa Chakavu ambapo kwasasa yapo katika hatua ya mwisho kukamilika ambapo yatafungwa vifaa vya kisasa ikiwemo AC, Chaji ya Simu, TV, Viti,  Bodi mpya, Taa, Side mirrors, Tairi, Vioo huku baadhi zikiwekewa Vyoo vya Ndani kwa lengo la kuweka mazingira Rafiki kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama" amesema

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya  Dar Coach LTD ambayo imejitolea kufanya Ukarabati huo Manmeet Lal amesema kuwa zoezi hilo ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha Ulinzi na usalama  wa Raia na mali zao kwa ujumla. Pia amemhakikishia Rc makonda hadi mwishoni mwa mwezi huu kumkabidhi magari matano ambayo yameshakamilika ambapo alisema jumla ya shilingi milioni 830 zimetumika kwaajili ya ukarabati huo.

Hata hivyo kwa upande wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar ea salaam Lazaro Mambosasa,amemshukuru Rc makonda kwa hatua aliyoichukua kusaidia vyombo vya ulinzi na usalama kupitia wadau wake kusaidia kukarabati mabasi hayo ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

IMG_3944
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishikana mikono  na Meneja Mauzo wa Kampuni ya Babasi ya Scania Hanif Ally,walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara  kwenye Kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza,  ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa mwengine (kulia) ni mmoja wa Maofisa wa kampuni ya Scania Deogratias Kabeho. 
 IMG_3945
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul MakondaA akishikana mikono na Mmoja wa Maofisa wa Kampuni ya Babasi ya Scania Deogratias Kabeho walipokutana wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara  kwenye Kampuni ya Dar Coach LTD, na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza,  ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.
IMG_3894
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Dar Coach Ltd Manmeet Lal (Sunny) wakati Mkuuwa Mkoa alipokwenda kufanya ziara  kwenye Kampuni hiyo na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi,Jeshi la Police na Magereza,  ambapo ameahidiwa hadi Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu baadhi yatakuwa yameshakamilika na kukabidhiwa.
1
Baadhi ya magari ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanaendelea kutengenezwa ambayo yalipelekwa yakiwa yameharibika kabisa 

2
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza leo wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati alipoenda kukagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayotengenezwa na Kampuni ya  Dar Coach. 
3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo leo na Mkurugenzi wa kampuni ya Dar Coach Manmeet Lal kuhusu hatua waliyofikia katika kufanya matengenezo ya magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama
4
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikagua magari 11 ya vyombo vya ulinzi na usalama ambayo yanatengenezwa mabodi yake yaliyokuwa yameharibika.Matengenezo hayo yanafanywa na Kampuni ya Dar Coach Ltd
IMG_3874

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *