Sunday, January 21, 2018

Wateja sita wa Benki ya NBC wajinyakulia Suzuki Carry ‘kirikuu’ kampeni ya Malengo
Mkurugenzi
wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert
Mponzi (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya
Malengo ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Kampeni, Mtenya
Cheya na kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari
Maggid. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya Suzuki Carry
maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi hao ni Fatuma
Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe
wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda
ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika kampeni hiyo
iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda zawadi ya
pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja.
Meneja
wa Amana za Wateja wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (wa pili kushoto),
akichezesha droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo jijini
Dar es Salaam leo. Washindi sita walijishindia kila mmoja gari jipya aina ya
Suzuki Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ lenye thamani ya shs milioni 30. Washindi
hao ni Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi Chiwini wa Pwani,
Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda ya ziwa, Patrick
Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya kusini. Katika
kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu washindi wengine 24 walijishinda
zawadi ya pesa taslimu shs milioni 1 kila mmoja. Wengine kutoka kushoto
ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid, Meneja Kampeni ya
Malengo, Mtenya Cheya na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Meneja
Kampeni wa NBC, Mtenya Cheya (kushoto), akizungumza kwa simu na mmoja wa
washindi sita aliyejishindia zawadi ya Suzuki Carry maarufu ‘Kirikuu’ wakati wa
droo kubwa ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa
Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi (wa pili kulia ),
akizungumza wakati wa droo kubwa ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC jijini
Dar es Salaam leo ambapo NBC imetoa zawadi
zawadi ya gari aina ya Suzuki Carry 'Kirikuu' kama inavyoonekana moja ya gari
hilo (kushoto) likionyeshwa kwa waandishi wa habari wakati wa droo hiyo.
Na Mwandishi Wetu.
WATEJA sita wa Benki ya NBC
wameibuka kidedea baada ya kila mmoja kujishindia gari jipya aina ya Suzuki
Carry maarufu kama ‘Kirikuu’ katika droo
kubwa ya Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam jana.
Kampeni hiyo iliyodumu kwa miezi
mitatu imeshuhudia wateja hao kutoka katika maeneo yaliyogawanywa katika kanda
sita nchini wakitangazwa washindi wa
magari hayo yenye thamani ya shs millioni 30 kila moja jumla yakiwa na thamani
ya shs milino 180.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkurugenzi
wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi
alisema kampeni hiyo iliyovutia waterja wengi wapya kujiunga ilishuhudia
washindi wengine 24 kupatikana katika droo mbili zilizofanyika katika miezi
miwili ya nyuma ambapo kila mmoja alijishindia zawadi ya pesa taslimu shs
milioni 1.
“Kampeni hii ya Akaunti ya Malengo ya NBC imekuwa na
mafanikio makubwa kwani tumeshuhudia zaidi ya akaunti mpya 6000 ziikifunguliwa
na wateja wetu wakihamasika kujiwekea akiba kwa malengo yao ya baadae”, alisema.
Alisema kampeni hiyo ilizinduliwa
mwaka jana kipindi ambacho NBC ilikuwa ikiadhimisha miaka 50 ya huduma bora kwa
wateja tokea kuanzishwa kwake.
Katika droo hiyo zawadi hizo za
Suzuki Carry sita ‘kirikuu’ zilikwenda kwa Fatuma Ramadhani kutoka kanda ya Dar es Salaam, Saidi
Chiwini wa Pwani, Lucina Massawe wa kanda ya kaskazini, Kelvin Machage wa kanda
ya ziwa, Patrick Mgimwa wa kanda ya kati na Fridino Benito kutoka kanda ya
kusini.
Hii ni mara ya tatu Benki ya NBC
kuendesha kampeni ya akaunti ya Malengo mara hii ikitoa zawadi zenye thamani ya
zaidi ya shs milioni 204 ambapo mwaka 2016 wateja wawili Aldo Nsuha mkazi wa Tabata Dar es Salaam na Lawrence Njozi kutoka Masasi
mkoani Mtwara wakijishindia magari mapya aina ya Toyota
Hilux double cabin.
Tags
# BIASHARA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
TPB YASAIDIA CHAMA CHA SKAUTI KUTENGENEZA DATA ZA KUTAMBUA WANACHAMA WAO
Older Article
RC MAKONDA AKOSHWA NA UTENDAJI KAZI WA KAMPUNI YA DAR COACH LTD
Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery
Hassani MakeroMar 11, 2025Benki ya NBC Yaandaa Hafla ya Futari Zanzibar, Yajivunia Ongezeko la Wateja
Hassani MakeroMar 07, 2025BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA RASHAL ENERGIES, INAYOJENGA BOMBA LA GESI KISEMVULE-MBAGALA
Hassani MakeroMar 07, 2025
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment