"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, March 12, 2025

"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank

Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania kupitua umoja wao uitwao ‘Red Skirts’ wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wagonjwa katika Hospitali ya CCBRT, baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa wa fistula kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, hospitalini hapo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Absa wakibeba msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti), kab;la hawajavikabidhi katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Anna Chacha (wa saba kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa tiba na vifaa muhimu vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) katika Hospitali ya Muhimbili kwa Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga, Dk. Martha Mkony, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkuu wa Ubora na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Emelda Lwena, kwa ajili ya wagonjwa wa fistula, kwenye jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

WATOTO wanaozaliwa na changamoto mbalimbali katika Hospitali ya Muhimbili, sasa wanaweza kupata ahueni zaidi mara baada ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya Absa Tanzania, kukabidhi msaada wa vifaa tiba na vifaa muhimu vya kusaidia watoto hao wanazaliwa kabla ya kufika wakati wa kujifungua.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga katika hospitali hiyo, Dk. Martha Mkony alitoa shukrani kwa wafanyakzi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanwake Duniani alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani utasaidia sana watoto wanaozaliwa kila siku katika hospitali hiyo.

Nipende kuwashukuru sana wanawake wa Benki ya Absa kwenye kundi lao wanalojiita ‘Red Skirts’ kwa tendo hili la kijamii, na tunajua hii ni mwanzo wa mahusiano marefu kati ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha watoto wachanga pamoja na Benki ya Absa na tunaahidi kushikiriana kwa pamoja katika kuwahudumia watoto wachanga”, alisema Dr. Marha.

Akizumgumza wakati akibidhi vifaa hivyo, Meneja katika Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Absa, Bi. Martha Chacha alisema, kwa kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa, pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, wanawake wa Benki ya Absa Tanzania, kupitia umoja wao wa ‘Red Skirt’ walikwenda kutoa misaada kwa wagonjwa wa fistula katika Hospitali ya CCBRT pamoja na kitengo cha Watoto Njiti katika Hospitali ya Muhimbili.

Kwa niaba ya wanawake wenzangu tupo mahali hapa tukiwakisha benki yetu kutoa misaada hii, Benki ya Absa inajali Story za Wanawake wa Tanzania, Story za mafanikio ya kiafya na kiuchumi kwa wanawake zina umuhimu sana kwetu”, aliongeza Bi. Anna

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages