
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 12, 2025 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Majisafi ya Ziwa Victoria kutoka Makomero - Mgongoro, uliopo kijiji cha Mwamayoka, Igunga mkoani Tabora ambao umegharimu shilingi milioni 840.8
Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo, ambao unatarajia kuhudumia wananchi 5,402, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali
Inaendelea kusimamia utoaji wa huduma za maji safi na salama nchini ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji inawafikia wananchi kwa asilimia 100
“Ndugu zangu wananchi, mradi huu ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, kuweni na uhakika kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi anayewajali, anawapenda na anasikiliza changamoto zenu, endeleeni kutekeleza majukumu yenu ipasavyo kwasababu tunaye kiongozi madhubiti”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza RUWASA kuongeza na kusogeza vituo vya kuchotea maji karibu na wananchi “RUWASA hakikisheni miradi hii inatoa maji wakati wote”
Mradi huo ambao umefikia asilimia 80 ya ujenzi unahusisha ujenzi wa vituo sita vya kuchotea maji, Ukarabati wa vituo sita vya kuchotea Maji, Ukarabati wa Manywesheo mawili ya Mifugo, kuchimba mitaro ya kulaza bomba na kufukia mitaro mita 25,000
Mheshimiwa Majaliwa yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.




No comments:
Post a Comment